Mbulu: Wanusurika kuuawa na gari lao kuteketezwa baada ya kudhaniwa ni watekaji wa watoto

Mbulu: Wanusurika kuuawa na gari lao kuteketezwa baada ya kudhaniwa ni watekaji wa watoto

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798

Watu wanne wamenusurika kifo baada ya kupigwa na kukatwa mapanga pamoja na gari waliyokuwa wakiitumia aina ya Raum kuchomwa moto katika Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara kwa kudhaniwa kuwa ni wezi wa kuiba Watoto baada ya kumpa pipi Mtoto aliyekuwa akipita pembeni ya gari yao waliyokuwa wanaitumia.

Neema Kilai ambaye alikuwa kwenye gari hiyo amesema kuwa walikuwa wakitoka kwenye harusi katika kijiji cha Kidarafa katika shughuli ya kupika ambapo gari yao ilipata pancha ghafla waliona gari yao ikiwa imezungukwa na walipofika pale waliambiwa kuwa wao ndio wanahusika kuwakata Watoto viungo.

Amesema kuwa Wananchi hao wakiongozwa na baadhi ya Viongozi walianza kuwashambulia kwa mapanga na mawe na kisha baadaye kuanza kuichoma gari hiyo.

“Kwenye gari tulikuwa tumebeba mahindi, jogoo wawili tumepewa, kuna njiwa, kuna begi zetu na nyama, pipi zilikuwa za kwetu tulikuwa tumenunua tunatafuna, Mtoto alivyopita akatuona tunakula yule rasta akampa kidogo Mama yake akatokea akawa anamchapa yule Mtoto yule wifi wangu akauliza mbona unamchapa Mtoto hivyo?akamuambia haikuhusu wakaanza kuongezeka, walituambia tuvue nguo zote ila Kaka yangu akasema kuliko nivue bora mniue”—— Neema

Watu wawili kati ya wanne wametibiwa katika Hospitali ya Meru lakini wengine wawili ambao ni Mke na Mume wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Chanzo: Millard Ayo

Pia soma
 
Hii kitu nlisema na itakuja tokea
Watu watakuwa wanakaa kimachalemachale,kuviziana

Ova

Sure mimi napendekeze wananchi wawe makini na watu wa design kama hao maana moyo wa mtu ni kichaka ,kihalisia haiwezekani umpe mtoto pipi ambaye hata haumjui.

Maisha yamebadilika hata kama mtu unamdai pesa jitahidi umpigie simu na si kumfuata kwake au sehemu na kuanza kumdai maana akiita tu mwizi umekwisha.

Kwa vijana kwenda kwenye maghetto au hostel kwa madada bila appointment nayo ni hatari sana ,ukimfuma na sponsor lazima akuitie mwizi.
 
Mkiambiwa mnunue bunduki mnasema ooh mimi nigawa pipi kwa watoto na mtu ajichanganye mamaae namlima bunduki ya pumbu natawanya kengele
 
Dah pipi imezua mambo😭😭😭wema wao umewaponza
 
Wao ni watu wa catering hao njiwa kuku na mahindi wakiokuwa kwenye gari wa kazi gani?

Polisi iwachunguze hao majeruhi kuna ukakasi hapo
 
Hatari sana ,hii inatuogopesha sisi wenye moyo wa kusai kusaidia watu,wema wao unewaponza,ila si vizuri kumpa kitu mtu usiyemjua tena chakula,ni hatari sana
 
Back
Top Bottom