Mbulu: Wanusurika kuuawa na gari lao kuteketezwa baada ya kudhaniwa ni watekaji wa watoto

Somo kwa the so called wasiojulikana. Hivyo ndivyo wanavyotakiwa kufanyiwa
 
Pole yao lakini hao jamaa wajinga sana. Unaanzaje kumpa mtoto wa mtu pipi huku humjui wala hakujui? Wacha wapigwe tu.
Mimi hapa hata lifti tu kwenye baiskeli yangu ya swala hupati kama sikujui japo nitakuhurumia tu kwa kutembea.
 
Wao ni watu wa catering hao njiwa kuku na mahindi wakiokuwa kwenye gari wa kazi gani?

Polisi iwachunguze hao majeruhi kuna ukakasi hapo
Mi sijaelewa, kuku na mahindi kwenye gari wa kazi gani?

Kwenye gari ilitakiwa wakutwe na nini? Kondom?
 
Serikali isipokua serious kutoa elimu kwa wananchi wetu tutaendelea kuwa na raia bogus milele
 
Sometimes kujichukulia sheria mkononi ni ushamba
Yees; But Sometimes ni ujasiri pia. Kama anayetakiwa kuilinda Sheria iliyopo anazembea, basi huna budi wewe ujichukulie hiyo Sheria mkononi mwako. Mazungumzo ni baadaye.
 
Kumpa mtoto pipi isn't a big deal.
Mbona mie kuna muda nakula chakula na watoto siwajui??
Muda mwingine kujichukulia sheria mkononi ni ushamba.
Je uchunguzi ukifanyika na ikagundulika hao watu hawana makosa??
Mtawafidia kwa namna gani??
Je mmoja wapo angepoteza maisha??
Mngemfidiaje??
Kama wao wangekua wana shauku wangewakamata na kuwafikisha mikono ya sheria na taratibu zingine zinafuata.
Yani mimi ndio niwe muhanga ndugu yangu kaumizwa na hana hatia kisa eti umachale wa wanakijiji!!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nitaanza na mwenyekiti aliyewaongoza kuyaondoa maisha yake pasi na kupepesa jicho.
 
Sio ushamba , jaribu kufikiria watoto wanatekwa Kila Leo na polisi analeta masihara kwann usiingie field mwenyewe.
Je kama waliodhurika hawana hatia?
Utawafidiaje?
Sio tu ushamba ni usenge kabisa.
Kama wao walikua na mashaka nao kwanini wasingewakamata na kuwafikisha kituoni kwa uchunguzi zaidi!??
 

Kwa kudhaniwa..

Aina za kina Stroke uhalisia wao umejengwa kwenye kudhania.

Hao ndiyo wanaotuletea hii medali adhimu!

 
Wao ni watu wa catering hao njiwa kuku na mahindi wakiokuwa kwenye gari wa kazi gani?

Polisi iwachunguze hao majeruhi kuna ukakasi hapo
Kipondo na mapanga wamechezea hao watu wa catering,chupuchupu watolewe uhai uwatoke

Ova
 
Tuwe na utaratibu wa kuhoji watu. Wawekeni chini wahojini wametoka wapi kwa nanni na wametoka kufanya nini,wanakwenda wapi wana nini kwenye gari na mnakagua kama ni watu waovu mtawajua tu.

Usiende sehemu ukakuta watu wanapiga nawewe ukapiga tu tue na tabia ya kudadisi vitu kwanza. Tubadilike WATANZANIA!!!
 
Wameshindwa kufanya uchunguzi kugundua watekwaji walipo sembuse wachunguze hilo?
Dhamana ya kulinda familia zetu sahivi iko mikononi mwetu.

Nawasapoti hao wananchi
 
Pole yao lakini hao jamaa wajinga sana. Unaanzaje kumpa mtoto wa mtu pipi huku humjui wala hakujui? Wacha wapigwe tu.
Mimi hapa hata lifti tu kwenye baiskeli yangu ya swala hupati kama sikujui japo nitakuhurumia tu kwa kutembea.
Kwakua hakukua na ndugu yako sio. Kuwapa watoto vijizawadi umekua utamaduni wa kiungwana wa Watanzania bila kujali ni mwanao ama lah unaweza kua na biskuti pipi bigijii na ukaona watoto wanacheza ukawapa kwa upendo tu isiwe sababu ya mtu kupigwa. Tue na tabia za kuhoji watu kama unaona kua humuamini mhoji very simple.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…