Pre GE2025 Mbunge Abood ashiriki kuchimba barabara na Wananchi kwa majembe ya mkono

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
SIMPONGEZI. Alishindwa kuleta mashine zifanye hiyo kazi kwa muda mfupi ili wananchi wafanye shughuli zingine za maendeleo? Halmashauri haina fungu la kurekebisha hiyo barabara?
 
Dharau Sana
Municipal Haina Maji, Barabara, Viwanda Vimekufa, Vingine Anafugia
CCM Itupishe Sasa
 
So what?! Kutembea na kobazi ndo ilkua agenda zake kipnd anaomba ubunge?!
 
Ndivyo inavyotakiwa, si kama wabunge wa mjini, wamejigeuza wafalme, huwakaribii kirahisi
 
Waluguru ni kikwazo kikubwa sana cha maendeleo ya mji wa Morogoro huwa hawakumbuki wanavyodharauliwa na hao wanasiasa wakitoka tu hapo wanapewa vipande vya nyama, mafuta ya kula, mchele na sembe hakumbuki tena madhila yoyote. Ukitokea msiba wanapewa usafiri na sanda kwishineey

Hapo Morogoro kuja kuleta maendeleo yatakiwayo ni sharti apatikane Mbunge ambaye sio tajiri na mfanyabiashara mwenye asili ya mikoa mingine kwa utetezi ufuatao
1. Maji (hakuna uhakika wa maji Kihonda, Mkundi, Makunganya, Kingolwira)
2. Kuimarisha miundo mbinu ya barabara za kudumu (lami) na kupanuliwa kuanzia Mzumbe-Msamvu (njia nne), Mikese-Msamvu (njia sita), Makunganya-Msamvu (njia sita)
3. Ardhi (makazi, mashamba ya mkonge ya magereza yahamishwe Kingolwira, Mkambarani na Kihonda)-wananchi wapewe mashamba ya kilimo wilaya ya Mvomero
4. Umeme (pamoja na kwamba umeme unazalishwa Kidatu, Kihansi na bwawa la Nyerere lakini hakuna uhakika wa umeme na pale wanaoweza kuunganishiwa bei iko juu na ukiritimba mrefu sana mpaka unapata zaidi ya gharama halisi zilizopangwa)
5. Mpango mji wa kisasa
6. Huduma za afya kusogezwa Kihonda au Mkundi, Mikese, Kichangani, Lukobe na Kingolwira
7. Huduma za kijamii kama shule, masoko ya wafanya biashara wadogo njia ya Iringa, Dar Es Salaam na Dodoma inatakiwa kuchukuliwa kwa umuhimu wa kwanza ili kuboresha kwa maendeleo ya kiuchumi
8. Bwawa la maji maeneo ya Kiegea linatakiwa kupanuliwa na kuimarishwa ili lisaidia kupunguza kama sio kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji maeneo ya Kihonda, Mkundi, Vespa hadi kituo cha SGR kwa Cha Chambo
 
Hivi kwa mtu mwenye akili timamu zama hizi ni za kuchiimba barabara kwa jembe la mkono tena makao makuu ya mkoa! Hayo ni matusi makubwa
 
Anaonyesha wananchi kuwa yeye aweza maisha aina zote na aweza saidiana na wananchi wa aina zote na kazi zote
Nawe unaamini!! Mleta hoja naye kama vile anamsaidia kum-promote, kama vile anashangaa Tajiri kuingia peponi!! Badala ya kulipia greda kuwasaidia, tena kw brbr zote, anatoka akiambatana na fotografa wake kuja ktk kampeni ...loh!
 
Nawe unaamini!! Mleta hoja naye kama vile anamsaidia kum-promote, kama vile anashangaa Tajiri kuingia peponi!! Badala ya kulipia greda kuwasaidia, tena kw brbr zote, anatoka akiambatana na fotografa wake kuja ktk kampeni ...loh!
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hii ndio bongo usanii tu...basi masikini na fukara wakiona hivyo wanashangilia sana wakijua ni mwenzao kumbe ni msanii tu.
 
Moro wao wanaridhika mambo madogo mno.
 
Chukuwachakomapema katika UBORA WAO!
Raia huko usistaajabu kumpigia kura badala ya kuomba matrekta, scaveter nk nk!
Bure kabisa kabisa kabisa 🤬 🤬 🤬 🤬 🤬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…