Mbunge adai SGR itajengwa kwa miaka 81

Staili hii si JPM aliikataa kwenye bandari ya bagamoyo?
 
Plan ya Funding ya huu mradi JK aliishaiweka sawa kabla ya kustaafu, mambo yalikuwa yanaenda vizuri. Kaja huyu JPM kaleta ujuaji wake sasa tunahangaika kutafuta hela, na safari hii kwa sababu project tumeshaianza na Wahisani wanajua kuwa tunashida kwa sababu hatuwezi kuacha tena watatupiga mariba makubwakubwa

Huu mradi mpaka unaisha tutajikuta tunatumia hata 50% more kuliko makadirio ya awali, na hii ni disaster
 
Na wewe uwe unajifunza na kufuatilia mambo kwanza, kabla ya kuandika.
Suala la kuwepo malipo ya serikali kimtandao (govenment e-payment) ambayo ndio imezaa hiyo Control number ni mfumo uliofanyiwa utafiti na kupitishwa kutumika kipindi cha Kikwete japokuwa ulianza rasmi kutumika kipindi cha Magufuli. Majaribio yake yote yamefanyika kipindi cha Kikwete.

Ni kama ilivyo mradi wa SGR ulipitishwa kipindi cha Kikwete, hakupatikana mtu wa kuweza kuufadhili kipindi kile, Magufuli akaanza kuujenga na kama utakuja kukamilika kipindi cha mama Samia Suluhu basi haitamaanisha ni mradi wa Mama Samia.

Yote kwa yote, bado wataalamu wanasema bado kuna upotevu mkubwa wa malipo ya serikali kwa njia hiyo ya mtandao, mfumo wake wa kiusalama kimtandao ni hafifu, wajanja wa IT wanaweza kuingilia kirahisi na kupiga pesa. Hivyo unahitaji maboresho ya kimsingi.
 
Pole pole mawazo ya.kuturudisha nyuma yanaanza kupenyezwa.Okay,tusubiri,lakini Watanzania wana akili na wanaona.
 
Huo mradi hata ukikamilika hautakaa ulipe boss .. na ndio maana Ndungai alipendekeza PPP waingie ubia na kampuni binafsi kwenye uendeshaji
HEP ni Hydro Electric power
Ooh..I get it. Itafutwe namna be it PPP or any other modality tupate kupona...maana tukichanganya miradi yote iliyoanzishwa halafu iishie hewani jamani...hela yote ambayo imeshazama hapo...?!
 
Huyu Mbunge alikuwa wapi wakati Rais Magufuli alipokuwa hai hakumweleza. Wamwache Mrithi wake Mhe. Samia Suluhu Hasani akamiliche miradi aliyoachiwa na Mtanguluzi wake. Acha hofu, hofu ni mbaya sana.
 
Itafika sababu mpaka sasa hiyo phase 1 haijakamilika na ni miaka minne sasa tunaelekea wa tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…