Mbunge Agnesta Kaiza: Jimboni kwangu Segerea, mvua zikinyesha barabara nyingi hazipitiki

Mbunge Agnesta Kaiza: Jimboni kwangu Segerea, mvua zikinyesha barabara nyingi hazipitiki

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Agnesta Lambert Kaiza, kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), amesema kuwa katika jimbo lake bado kuna kero kubwa ya barabara, hususan za ndani. Ameeleza kuwa mvua zinaponyesha, njia nyingi hazipitiki.

“Njia hazipitiki ndani ya Jimbo la Segerea, hasa zile za ndani, na hata barabara kuu nazo bado ni tatizo. Nyinyi ni mashahidi kama mnafuatilia hali ya Jimbo la Segerea, mvua zikinyesha, mara nyingi kunakuwa na mafuriko,” amesema.

Hayo ameyasema Februari 26, 2025, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. Alieleza kuwa yeye, kwa kushirikiana na madiwani, wataendelea kuweka msukumo ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mdau wa JamiiForums.com alidai kuwa katika Mtaa wa Twiga uliopo Segerea kuna kero ya barabara kipindi cha mvua, ambapo alitoa rai kwa Mbunge na mamlaka husika kuchukua hatua.

“Rai yangu kwa Mbunge wa Jimbo la Segerea ni atusaidie kufikisha sauti yetu kwa mamlaka husika ili barabara hii iweze kuboreshwa na kuondoa kadhia tunayoipata, hasa katika vipindi vya mvua. Pia, mamlaka zikiona taarifa hii, zifuatilie na kuchukua hatua ili kutuepusha na kero hii,” alisema mdau huyo.

Mjadala mwingine soma ~ Dar: Wananchi Mtaa wa Twiga (Segerea) tunateseka kwa ubovu wa barabara hasa vipindi vya mvua
 
Back
Top Bottom