Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shabiby kaongea point. Ila wengi wetu hatujitambui. Mzee Ruksa alipotoa ruksa kwa mtu kufanya biashara aitakayo, nchi ya Tanzania ikabadilika, vitu vizuri vikaingia, nchi ikapiga hatua. Tukumbuke vizuri kabla ya ruksa tulikuaje? Na serikali ilikuwepo.Mhe. Ahmed Mabukhut Shabiby, Mbunge wa Gairo, juzi bungeni uliongea kwa uchungu saana wakati unachangia, lengo la mchango wako ilikuwa ni kuvunjwa kwa utaratibu wa kuagizwa kwa mafuta kwa pamoja (bulk procurement) na kisha kila mfanyabiashara mwenye uwezo wa kupata mafuta kwa bei anayoweza aende deep sea akanunue, kwa maana huko deep sea kuna meli zina mafuta zinashindwa kwa kupeleka na mfanyabiashara anaweza akanunua kwa robo ya bei ya dunia.
Mhe. Ahmed Mabukhut Shabiby, naomba nikukumbushe kuwa Tanzania sio pango la walanguzi na wala sio pango la wanyanganyi kuwa sasa Serikali iruhusu watu wabebe fedha taslimu(cash) waende deep sea wakaanze kununua kwa fedha taslim (ship to ship), Tanzania kama nchi imeingia mikataba ya Kimataifa, Tanzania kama nchi kuruhusu Wafanyabiashara wakanunue tu mafuta ambayo yawezekana mengine yamepokwa kutokana na yanayoendelea kati ya Vita vya Russia na Ukraine ni kuingia kwenye matatizo na jumuia za Kimataifa.
Mh. Ahmed Mabukhut Shabiby, ukiwa kama Mbunge, ni muda muafaka wa kuishauri Serikali kuhakikisha kama nchi tunaangalia namna bora ya kupambana na Inflation, ni kweli bei ya mafuta itaendelea kupanda na itasababisha bidhaa nyingi kupanda bei, kama ulivyo sema hakuna namna Serikali itatoa kodi ya mafuta, kodi ndio zinaendesha nchi, kodi ndio zinalipa mishahara, kodi ndio zinawezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Waambie Wana Gairo na Watanzania kwa ujumla ukweli juu ya hili. Tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta kwa sasa ni nchi zote duniani, hata majirani zetu wao wako vibaya kuliko Tanzania, lakini wewe kama Mbunge una nanafasi ya kuishauri Serikali ione namna bora ya kutoa ruzuku (subsidy) katika mafuta ili kupunguza upandaji wa bei ya mafuta
Mh. Ahmed Mabukhut Shabiby,ukiwa mmoja wa Wadau wa mafuta umezungumza kitu kikubwa saana juu ya kamati inayoshughulikia manunuzi ya pamoja ya mafuta (Bulk procurement), Imani yangu shutuma hizi hazijatoka kwa bahati mbaya, ni imani yangu una ushahidi na Serikali ya awamu ya sita haitaacha kushughulikia hili kupitia vyombo vyake, Imani yangu ukiwa mwakilishi wa Watanzania na mtu unayemsaidia Mama yetu Samia Suluhu Hassan ambaye usiku na mchana ana pambana kuhakikisha Tanzania ina rudi kwenye ramani na Watanzania wanafaidi matunda yao, jambo hili utalipeleka Takukuru ili liweze kushughulikiwa mara moja.
Rai ya ngu kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania wamewatuma mkamsaidie Mheshimiwa Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusukuma gurudumu hili la Tanzania kusonga mbele, Mama yetu amekuwa akizunguka kote duniani kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo ambayo wamekuwa wakiyaota toka Tanzania ipate uhuru, ni jukumu lenu kumsaidia, na kama UTARATIBU WA KUNUNUA MAFUTA KWA PAMOJA UMEKUWA UKIWAUMIZA WATANZANIA , HAUNA TIJA KWA SASA,MNAYO NAFASI YA KUBADILISHA, mmefanya hivyo hapo nyuma kwa baadhi ya sheria ambazo zilionekana hazina manufaa kwa Watanzania.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN
Katika makosa yaliyofanyika issue ya Korosho ilikuwa kosa kubwa saanaHakuna Rais alikuwa anakurupuka kama Magufuli kwa taatifa yako. Usijifanye umesahau sakata la biashara ya korosho
Uliza Wapinzani wanaishije huko, then ndio utajua hujuiUlishawahi Kusikia Kagame Anaupiga Mwingi?View attachment 2181519
Hakuna Rais alikuwa anakurupuka kama Magufuli kwa taatifa yako. Usijifanye umesahau sakata la biashara ya korosho
Hiyo Nia njema ni wajinga tu ndiyo waliyoionaMaamuzi yake yote alifanya kwa nia njema…
HatariHaya mafisadi yanakuwaje viongozi kwenye nchi yetu hii nani atatuokoa?
Mkuu, unazungumzia kitu gani hasa, maanake umezungukazunguka sielewi hasa hoja yako ni nini? Mama Samia, au?MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN
Na kwa sasa wakubwa hao wanawasoma tu na vikura vyao vya 'kutofungamana'.Na wajanja hawaoni kuwa Shabibu anaishauri serikali iwaruhusu wafanyabiashara wa mafuta wakafanye money laundering huko deep sea. Mtegemee NATO wakisikia hivyo waendelee kuwaletea fedha za makali ya uviko? Mtaambulia vikwazo na hii hali ngumu inayosababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa Taifa litatikiswa haswa.
Mwamba kabisaHuyu mwamba alikuwa mchapa kazi aisee…wakati huu mgumu angetutetea wanyonge
!!Huu uzi siyo wa February Ma rope mwenyewe kabisa huu?
Asipokaa sawa atatengenezewa kashfa imuue kisiasa.hoja ya shabiby inatishia ulaji wa 10% ya wanakamati kwahiyo tutalajie mfululizo wa mabandiko hala.
Huyu mwamba alikuwa mchapa kazi aisee…wakati huu mgumu angetutetea wanyonge
Mkuu, unazungumzia kitu gani hasa, maanake umezungukazunguka sielewi hasa hoja yako ni nini? Mama Samia, au?
Maneno meeeengi, lakini 'substance' hakuna!