Mbunge Ahmed Mabukhut Shabiby: Tanzania sio pango la Wanyang'anyi

Mbunge Ahmed Mabukhut Shabiby: Tanzania sio pango la Wanyang'anyi

Tanzania haiwezi kukosa kuwa pango la wanyang'anyi kwa kuwa wapangaji CCM ni wanyang'anyi.
 
Mhe. Ahmed Mabukhut Shabiby, Mbunge wa Gairo, juzi bungeni uliongea kwa uchungu saana wakati unachangia, lengo la mchango wako ilikuwa ni kuvunjwa kwa utaratibu wa kuagizwa kwa mafuta kwa pamoja (bulk procurement) na kisha kila mfanyabiashara mwenye uwezo wa kupata mafuta kwa bei anayoweza aende deep sea akanunue, kwa maana huko deep sea kuna meli zina mafuta zinashindwa kwa kupeleka na mfanyabiashara anaweza akanunua kwa robo ya bei ya dunia.

Mhe. Ahmed Mabukhut Shabiby, naomba nikukumbushe kuwa Tanzania sio pango la walanguzi na wala sio pango la wanyanganyi kuwa sasa Serikali iruhusu watu wabebe fedha taslimu(cash) waende deep sea wakaanze kununua kwa fedha taslim (ship to ship), Tanzania kama nchi imeingia mikataba ya Kimataifa, Tanzania kama nchi kuruhusu Wafanyabiashara wakanunue tu mafuta ambayo yawezekana mengine yamepokwa kutokana na yanayoendelea kati ya Vita vya Russia na Ukraine ni kuingia kwenye matatizo na jumuia za Kimataifa.

Mh. Ahmed Mabukhut Shabiby, ukiwa kama Mbunge, ni muda muafaka wa kuishauri Serikali kuhakikisha kama nchi tunaangalia namna bora ya kupambana na Inflation, ni kweli bei ya mafuta itaendelea kupanda na itasababisha bidhaa nyingi kupanda bei, kama ulivyo sema hakuna namna Serikali itatoa kodi ya mafuta, kodi ndio zinaendesha nchi, kodi ndio zinalipa mishahara, kodi ndio zinawezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Waambie Wana Gairo na Watanzania kwa ujumla ukweli juu ya hili. Tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta kwa sasa ni nchi zote duniani, hata majirani zetu wao wako vibaya kuliko Tanzania, lakini wewe kama Mbunge una nanafasi ya kuishauri Serikali ione namna bora ya kutoa ruzuku (subsidy) katika mafuta ili kupunguza upandaji wa bei ya mafuta

Mh. Ahmed Mabukhut Shabiby,ukiwa mmoja wa Wadau wa mafuta umezungumza kitu kikubwa saana juu ya kamati inayoshughulikia manunuzi ya pamoja ya mafuta (Bulk procurement), Imani yangu shutuma hizi hazijatoka kwa bahati mbaya, ni imani yangu una ushahidi na Serikali ya awamu ya sita haitaacha kushughulikia hili kupitia vyombo vyake, Imani yangu ukiwa mwakilishi wa Watanzania na mtu unayemsaidia Mama yetu Samia Suluhu Hassan ambaye usiku na mchana ana pambana kuhakikisha Tanzania ina rudi kwenye ramani na Watanzania wanafaidi matunda yao, jambo hili utalipeleka Takukuru ili liweze kushughulikiwa mara moja.

Rai ya ngu kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania wamewatuma mkamsaidie Mheshimiwa Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusukuma gurudumu hili la Tanzania kusonga mbele, Mama yetu amekuwa akizunguka kote duniani kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo ambayo wamekuwa wakiyaota toka Tanzania ipate uhuru, ni jukumu lenu kumsaidia, na kama UTARATIBU WA KUNUNUA MAFUTA KWA PAMOJA UMEKUWA UKIWAUMIZA WATANZANIA , HAUNA TIJA KWA SASA,MNAYO NAFASI YA KUBADILISHA, mmefanya hivyo hapo nyuma kwa baadhi ya sheria ambazo zilionekana hazina manufaa kwa Watanzania.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN
Shabiby kaongea point. Ila wengi wetu hatujitambui. Mzee Ruksa alipotoa ruksa kwa mtu kufanya biashara aitakayo, nchi ya Tanzania ikabadilika, vitu vizuri vikaingia, nchi ikapiga hatua. Tukumbuke vizuri kabla ya ruksa tulikuaje? Na serikali ilikuwepo.
 
Na wajanja hawaoni kuwa Shabibu anaishauri serikali iwaruhusu wafanyabiashara wa mafuta wakafanye money laundering huko deep sea. Mtegemee NATO wakisikia hivyo waendelee kuwaletea fedha za makali ya uviko? Mtaambulia vikwazo na hii hali ngumu inayosababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa Taifa litatikiswa haswa.
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN
Mkuu, unazungumzia kitu gani hasa, maanake umezungukazunguka sielewi hasa hoja yako ni nini? Mama Samia, au?

Maneno meeeengi, lakini 'substance' hakuna!
 
Na wajanja hawaoni kuwa Shabibu anaishauri serikali iwaruhusu wafanyabiashara wa mafuta wakafanye money laundering huko deep sea. Mtegemee NATO wakisikia hivyo waendelee kuwaletea fedha za makali ya uviko? Mtaambulia vikwazo na hii hali ngumu inayosababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa Taifa litatikiswa haswa.
Na kwa sasa wakubwa hao wanawasoma tu na vikura vyao vya 'kutofungamana'.

"Either you're with us or you're not",; na nijuavyo viongozi hawa wa kwetu, haichukui raundi kudondoka chini na kulamba miguu!
 
Serikali ifanye hima kwenye haya;
1. CNG plant iharakishwe
2. Ianze fikiria kuanzishwa kwa plants kubwa za umeme mbadala

Dunia ilipo sasa, kuendelea kutegemea fossil energy ni kujikaanga na matokeo yake ndio kama haya ya bei ya mafuta kuyumbayumba
 
Mkuu, unazungumzia kitu gani hasa, maanake umezungukazunguka sielewi hasa hoja yako ni nini? Mama Samia, au?

Maneno meeeengi, lakini 'substance' hakuna!


😄 uoga umewazidi wabongo mpaka mtu anashindwa kuweka hoja yako wazi…

Kwa mtazamo wangu nahisi anamsihi Shabiby asiachie hapo mchango wake bungeni awapeleke wapiga dili, kamati ya manunuzi ya mafuta Takukuru ili wachunguzwe….Mama anahitaji msaada wake afanye hima😄
 
Back
Top Bottom