Hilo la Lissu na ubinafsi hebu tuliweke pembeni, ni mawazo yako binafsi pia.
Hili la Chadema ni chama kikubwa, kinahitaji pesa kujiendesha hivyo lazima kishiriki uchaguzi, kwasababu hapo watapata ruzuku na michango ya wabunge kwaajili ya shughuli za chama, naona hapo ndio umeandika pointi.
Lakini, hiyo pointi yako nakuja kuipinga kwasababu walishatuambia wana kitu kinaitwa Chadema digital, kwamba walikuwa na mpango wa kuwaandikisha wanachama milioni moja au zaidi nchi nzima, kisha hawa wanachama watapolipia kadi zao, basi chama kitapata pesa za kujiendesha, huu mpango wao sijui uliishia wapi.
Hapo utaona kwamba, Chadema na mapato sio lazima kushiriki uchaguzi, wana njia nyingine tofauti, kwangu mimi nionavyo zaidi, kushiriki uchaguzi kunakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa mbunge binafsi, zaidi ya chama chao, au hata majimbo wanayo bahatika kushinda.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app