Yah ni kweli kuwa nacheza bahati nasibu kwa kujaribu kuyajua mambo ambayo siko ndani yake.
Lakini katika dunia ya leo kuna njia na namna nyingi ya kujua mambo ambayo hauko ndani kwa kupitia vyanzo, dalili, sifa au kauli mbali mbali.
Ni mfano leo kuna asilimia kubwa ya wapinzani ambao hawaamini kuwa Zito ni mpinzani wa kweli. Sio kwamba wanajua kilichopo katika moyo wake, au labda yeye mwenyewe ashawahi kuwambia kuhusu hilo, bali wanasema hivyo au kuhisi hivyo kutokana na mwenendo wake na kauli zake.
So kufahamu kitu au jambo fulani sio lazima mpaka wewe uwe miongoni mwa hicho kitu. Bali unaweza kutumia akili na fikra kwa mbali kuliona jambo ambalo wengine hawalioni.