Mbunge aliyedai waongezewe mshahara atakiwa aachie jimbo, CCM nao watoa kauli

Ukileta hoja za kijinga unategemea majibu gani yanayolenga hoja zako ya kijinga?Upo msemo wa Kingereza usemao,"foolish answers for foolish questions."
 
Kuleana ndiko kunakoliangamiza taifa, kwanini yeye hakutumia hekima kuomba nyongeza ya mshahara huku akijua mwalimu anapata laki 3 kwa mwezi wakati yeye anaipata kwa siku.
Mwalimu kulipwa laki 3 siyo kosa la huyu mbunge, ni la mfumo. Na kosa hili la kimfumo halimzuii yeye kudai nyongeza ya mshahara wake.
 
ZAO la UCHAFUZI wa UCHAGUZI MKUU 2020
 
Umesahau kuwa wabunge wenzie walimpigia makofi ya mikono na miguu na kushangiliwa. Unataka tupoteze tena mda wa kusikiliza kisichoendana na uhalisia
Sasa kwann chongolo anamtolea maneno ya kibabe kiasi hiki. Hajui nyuma ya kauli hii Kuna robo tatu ya wabunge wa chama chake?
 
Hawa ni wabunge waliopitishwa na mwendazake baada ya wizi wa kura.
 
Hajahukumiwa bado; kesi yake iko kwa wananchi hadi 2025 ndipo hukumu utajionea mwenyewe, kama ndiyo shida yako.
 
wengi sana hapo futa Special seats wote ,futa nominated by PRESIDENT wote ,punguza majimbo 170
Haya nitafanya hivyo bosi wangu, kama ni rahisi tu kiasi hiko -- Kufuta!!! Kufuta!!! Kufuta!!! Nawaambia njoeni tarehe 1 Julai tuandamane Bi Mkubwa katuharibia nchi, mnabaki tu Jeiefu kutaipu sijui nini.

Unadhani waliopigana na Mzungu hadi akakimbilia kwao, wangefanya hivi tungekuwa na uhuru leo!???

Tokeni mje tuandamaneeeee mguu kwa mguu kutoka Newala Mtwara hadi Missenyi Kagera, kupitia Magogoni na Chamwino then Msoga.

Mwenge tutauzimia kuleee Butiama baada ya kuhitimisha kazi. Au nasema uongo ndugu zangu!???
 
Angejaribu huu ujinga wakati wa Jiwe "angefurahishwa"
Nahisi kama Sheria inayomtambua mbunge inamlinda kupindukia, it is as if akisha pata ubunge kinachoweza kumtoa bungeni ni kifo tuuuuuu
 
Alitakiwa kushusha nondo za kutetea maslahi ya mfanyakazi wa nchi hii bila kusahau mkulima, halafu ndo apandishe hoja yake ya maslahi ya wabunge.....utaona kabisa ubinafsi umemjaa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…