Mbunge Aloyce Kwezi Azindua Shule Iliyojengwa kwa Tsh. Milioni 398

Mbunge Aloyce Kwezi Azindua Shule Iliyojengwa kwa Tsh. Milioni 398

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Mhe. Aloyce Kwezi amezindua Shule ya Usimba Sekondari iliyopo katika Wilaya ya Kaliua ambapo aliambatana na Diwani wa Kata ya Usimba Ndugu Masanja E. Msonde.

Wakazi wa Kata ya Usimba walijitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Sekondari hii ambayo itawapa manufaa watoto waliokuwa wakienda umbali mrefu kwa ajili ya kupata elimu.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Usimba walitoa sifa kwa Mbunge Mhe. Aloyce Kwezi kwa kutoa kipaumbele katika Sekondari hiyo ambayo itaongeza kiwango cha elimu katika maeneo hayo.

Miezi kadhaa nyuma Serikali ilitenga kiasi cha fedha Tsh Milioni 398,000,000/= kwa ajili ya upanuzi wa kidato cha 5 na 6 katika Shule ya Usimba Sekondari

Usimba ni Kata ya Wilaya ya Kaliua katika Mkoa wa Tabora, Tanzania. Hii ni miongoni mwa Kata zenye idadi ndogo ya watu katika Sensa ya Mwaka 2022 ambapo wakazi wa Kata ya Usimba walihesabiwa 6,436.

"Sasa ni Usimba na Elimu,Elimu na Usimba"
 

Attachments

  • Screenshot 2024-09-28 at 09-45-37 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-45-37 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    641.6 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-45-52 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-45-52 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    915.9 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-46-13 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-46-13 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    910.7 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-46-27 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-46-27 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    1.2 MB · Views: 4
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-46-40 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-46-40 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    1,008.7 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-46-54 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-46-54 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    886.6 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-09-28 at 09-47-10 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-28 at 09-47-10 Kaliua PlusTz (@kaliuaplustz) • Instagram photos and videos.png
    1.1 MB · Views: 4
Kuna wengine shule hizo hizo zinajengwa kwa billions of money! Mpaka wanagaragara kwenye matope!
 
Back
Top Bottom