Mbunge ataka kuwe na utaratibu wa kuchukua fedha M-Pesa, Tigo Pesa kwa watu wanaofariki na kuacha fedha huko

Mbunge ataka kuwe na utaratibu wa kuchukua fedha M-Pesa, Tigo Pesa kwa watu wanaofariki na kuacha fedha huko

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mbunge wa Viti Maalum, Judith Kapinga amesema watu wanaofariki na kuacha fedha kwenye mitandao kama Tigo pesa, M-Pesa, Airtel Money nk wanazinufaisha kampuni za simu huku serikali ikiwa haipati kitu.

Ameishauri serikali iweke utaratibu ili ndugu wa karibu waweze kudai fedha hizo na serikali kunufaika kwa upande mwingine ili mitandao ya simu isinufaike peke yao kutokana na fedha nyingi ambazo waliofariki huziacha.

Hili ni janga kubwa Tanzania. Hata kwenye financial institutions, ikitokea mteja amaefariki kwao wanaona kama ni fursa, ukifuatilia unazungushwa kama pia.

Na wakiona account iko dormant mda mrefu na ina mtonyo shazi wanaanza kuidokoa dokoa.
 
Msimamizi wa mirathi (ambaye huwa anathibitishwa na mahakama) anaweza kudai pesa kutoka kwenye makampuni ya simu hata bila kuwa na password za simu husika. Ili mradi ajue kuna salio la maana - vinginevyo anaweza kusumbukia salio la sh. elfu nne!

Ila ni wazi ni rahisi na haraka zaidi mwenza wa ndoa au mtu mwingine akijua password.
 
Mbunge wa Viti Maalum, Judith Kapinga amesema watu wanaofariki na kuacha fedha kwenye mitandao kama Tigo pesa, M-Pesa, Airtel Money nk wanazinufaisha kampuni za simu huku serikali ikiwa haipati kitu.

Ameishauri serikali iweke utaratibu ili ndugu wa karibu waweze kudai fedha hizo na serikali kunufaika kwa upande mwingine ili mitandao ya simu isinufaike peke yao kutokana na fedha nyingi ambazo waliofariki huziacha.

Kisheia Mpesa au Tigo pesa sio sehemu ya kutunzia pesa, watu walisha fanya ndo bank
 
Back
Top Bottom