Mbunge au Diwani, akifa au kuhama chama, achaguliwe mwingine wa chama kile kile na kamati ya Wilaya au Mkoa. How does this sound?

Mbunge au Diwani, akifa au kuhama chama, achaguliwe mwingine wa chama kile kile na kamati ya Wilaya au Mkoa. How does this sound?

Sawa, lakini hata Waziri Mkuu anachaguliwa na watu wa jimbo lake tu, lakini anakuwa Waziri Mkuu wa nchi nzima kwa msingi wa kuwa mbunge aliyechaguliwa na watu wa jimbo lake tu. At least in theory.

Point ni kwamba angalau amepitia kizingiti cha kuchagukiwa na wananchi kuwa mbunge.

Mtu wa kuteuliwa tu anaweza kuwa hajapitia kizingiti cha kuchagukiwa hata na mtu mmoja.
Umefafanua vema. Thanks..
 
..kuna wakati tulikuwa na Naibu Waziri ktk wizara ya ulinzi.

..sina kumbukumbu ya mara ya mwisho wizara hiyo kuwa na Naibu Waziri.
Mkuu, Je ni takwa la kikatiba au ni utashi tu wa Mh. Rais??

Je, ni Wizara yoyote ile inaweza isiwe na naibu waziri au ni MoD pekee??..
 
Kama ni cheo mimi nishakaa na naibu waziri wa ulinzi Seif Bakari tukafanya mazungumzo ya kujenga taifa.
Sikuwahi kumsikia huyu mtu wala cheo hiki, inawezekana kwa sababu nilikuwa bado mdogo sana..
 
Unauliza hakuna mtu aliye naibu waziri wa ulinzi sasa au hakuna cheo cha naibu waziri wa ulinzi?

Kama ni cheo mimi nishakaa na naibu waziri wa ulinzi Seif Bakari tukafanya mazungumzo ya kujenga taifa.

..baada ya Col.Seif Bakari, na Brig.Moses Nnauye nani mwingine amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri wa Ulinzi?

..Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa ni wizara ambayo haifuatiliwi na vyombo vya habari hivyo taarifa na kumbukumbu zake ni vigumu kuzipata.

Cc SIPENDI SIASA
 
..Naamini ni utashi wa Raisi kwasababu tuna historia ya kuwa na Manaibu waziri ktk wizara hiyo.
Okay. Asante sana mkongwe. Tuna mengi sana ya maana ya kujifunza kupitia watu kama nyie..
 
Eti wadau, hii itasaidia kupunguza matumizi kwa hizi third world countries kama Tanzania?? How does this sound..

Mfano: Kafa Magufuli, akaingia Philip Mpango bila gharama za uchaguzi..

~ SIPENDI SIASA ~
Mkuu JokaKuu unaweza ukatia neno lolote hapa..
 
Miaka ya nyuma nilishawahi kuwaza hivi, hasa ukiangalia gharama kubwa ya pesa za wananchi inavyotumika katika chaguzi ndogo. Lakini baadae nikaja kugundua kama ikiwekwa kuwa hivyo matokeo ni kuwa hao wabunge na madiwani watakua wanakufa kwa idadi kubwa sana kila mara, sababu hapa ni Africa kuna teknolojia na pia kuna umasikini hivyo walio karibu kiwania hizo nafasi wangechagua kuwaua walio madarakani ili wao waingie
Kwa hiyo Samia alimuua Magufuli kwa mantiki hii??..

Mkuu, unamuuaje mtu ilhali majina 11 yanapelekwa katika kamati na wewe muuaji hauna uhakika kama jina lako litapitishwa??..

This is insane ujue..
 
Katika hiyo teknolojia wapo wanaoua wengine bila hata kugombea nafasi ya kisiasa wala chochote kile. Kuhusu majina ya watu unayotaja hapa ni kama inaenda nje ya mjadala. Makamu wa Rais hawezi kuua Rais ili yeye awe Rais kwa sababu wote wawili tayari wapo madarakani
Kumtaja Samia na Magufuli ni kama mfano tu. Don't take it seriously..
 
Katika hiyo teknolojia wapo wanaoua wengine bila hata kugombea nafasi ya kisiasa wala chochote kile.
Kama kuuwawa kisa ubunge au udiwani, si unaweza kuuwawa baada ya kupigiwa na wana Jimbo au kamati ya mkoa??

What's the difference now??..
 
Bora kufanya uchaguzi wa nafasi inayoachwa wazi, ili kuepusha njama za mauaji ya vongozi na wananchi wapewe nafasi kupata na kuchagua mtu anayefaa kwa nafasi inayoshindaniwa.
 
Bora kufanya uchaguzi wa nafasi inayoachwa wazi, ili kuepusha njama za mauaji ya vongozi..
Kwani mtu akipigiwa kura na wananchi ndio hawezi kuuwawa?? JFK wa Marekani hakuuwawa yule??..
 
Back
Top Bottom