Mbunge Aysharose Awapa Faraja Wanafunzi wa Shule Maalum ya Wasichana Sekondari ya Solya, Manyoni

Mbunge Aysharose Awapa Faraja Wanafunzi wa Shule Maalum ya Wasichana Sekondari ya Solya, Manyoni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ametembelea Shule Maalum ya Wasichana Sekondari ya Solya na kuzungumza na Wanafunzi wa kike shuleni hapo na kuwapa zawadi ya taulo za kike na vifaa vya michezo

Mbunge Aysharose Mattembe amewatia moyo Wanafunzi wa kike wanaosoma katika Shule Maalum ya Sekondari Solya huku akiwapa hamasa wanafunzi hao na amewasisitiza kusoma kwa bidii na kuzingatia lengo lililowaleta shuleni hapo na hatimaye kutimiza ndoto zao

"Nyie ndio wanafunzi waasisi wa Shule hii, hivyo mnatakiwa kuwa mfano bora kwa kufaulu vizuri ili kuwapa hamasa wadogo zenu ambao watajaliwa kujiunga na Shule hii hapo baadaye. Nataka kuona ufaulu wa daraja la kwanza kwa nyie wote" alisema Mhe. Aysharose Mattembe,

"Nikiwatizama hapa naona wote mnaweza tena mnaweza sana nataka msome kwa bidii ili baadaye mje kuwa viongozi wakubwa kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na mhe Spika Tulia Ackson ambaye pia ni Rais wa mabunge Duniani inawezekana kabisa endapo mtaweka juhudi kubwa katika masomo yenu na kuzingatia maadili" alisisitiza Mhe. Mattembe

Pia, Mhe. Aysharose Mattembe alimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Shule nzuri Watoto wa Singida kwani Shule hiyo maalum ni miongoni mwa Shule kumi za vipaji zilizojengwa nchi nzima na Singida ikiwemo.

Mwalimu Mkuu, Zainab Mtinda awali akisoma risala yake alimshukuru Mhe. Aysharose Mattembe kwa kuwajali, Zainab alisema kwa kuwa Shule ni mpya na ipo mbali na maduka ya Stationary, wana changamoto ya ukosefu wa Photocopy, Computer 3 na Maabara za Biolojia, Fizikia na Kemia hazina vifaa vya kutosha vya kujifunzia.

WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.11(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.12.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.17(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-22 at 17.18.17.jpeg
 
Back
Top Bottom