Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Umoja wa Wazazi Taifa CCM - Mbeya Mhe. Bahati Keneth Ndingo kwa kushirikiana na Haji Manara ambaye alisoma Shule ya Wazazi Chimala Secondary iliyopo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya pamoja na Wadau mbalimbali wa Mbarali Mkoani Mbeya wamefanikisha harambee ya ukarabati wa madarasa na mabweni ya Shule hiyo kwa kukusanya Tsh.14,588,000 ambayo imevuka lengo la kukusanya sh 12,777,000 kwa awamu ya kwanza.
Mhe. Bahati Keneth Ndingo ameahidi kushirikiana na kamati ya ujenzi mpaka mwisho huku Haji Manara na Wadau wengine wakiahidi kusaidia Shule hiyo mpaka ukarabati utakapokamilika.
Haji Manara amechangia Tsh. Milioni moja huku akiahidi kuipa Shule hiyo mashine ya photocopy yenye thamani ya Tsh. Milioni mbili, huku Madiwani wakitoa sehemu ya posho zao kuchangia ukarabati huo.
Hii ni awamu ya kwanza ya harambee hiyo ambayo bado itaendelea katika awamu ya pili, wengine waliochangia awamu ya kwanza ni Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Francis Mtega.