Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE BYABATO AWAFARIJI WATOTO YATIMA 200 KUPITIA TAMASHA LA BUKOBA MJINI MPYA 2024
📌 Lengo ni kuwapa faraja katika msimu wa sikukuu
📌 Vitabu, Madawati, Vitanda vyatolewa
📌Wananchi wajitolea kuchangia Damu
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephen Byabato, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wamewakutanisha watoto yatima wapatao 200 wanaoishi katika vituo vya Watoto Yatima katika Manispaa ya Bukoba kwa lengo la kuwapa faraja katika kipindi cha Msimu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.
Kupitia Bukoba Mjini Mpya Festival, Mbunge Byabato na Wadau wametoa vifaa vya shule, vyakula na mahitaji binafsi ikiwa pia ni sehemu ya sadaka na shukrani kwa Mwenyezi Mungu.
Tamasha hilo limefanyika tarehe 14/12/2024 kwa jitihada za wadau wa Kundi Songezi (WhatsApp Group) la Bukoba Mjini Mpya chini ya ulezi wa Mhe. Byabato na wadau nje ya kundi hilo.
Katika maandalizi ya tamasha hilo, zaidi ya Tsh 10 Milioni zilitolewa na wadau na leo wamekabidhi sadaka mbalimbali kwa watoto yatima zikiambatana na tuzo za utambuzi kwa waanzilishi na vyeti vya shukrani kwa wasimamizi wa vituo hivyo kwa kazi kubwa ya kuijenga Jamii bora ya Bukoba.
Pia vimetolewa Vitabu Vitakatifu vya Mungu (Biblia na Quran), madawati 50 kwa shule za msingi zenye uhitaji zaidi za Byabato, Bilele, Rwamishenye na Bunena.
Wananchi kutoka kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba wameunga mkono tamasha hilo na wengine kujitolea kwa kuchangia Damu, zoezi lililoendeshwa na hospital ya Mkoa wa Kagera.
Aidha katika kuunga jitihada za Mbunge Byabato, Mdau kutoka Afrika Kusini, Injinia Datusi, ametoa vitanda 20 kwa watoto yatima, huku wafanyabiashara wa Soko Kuu Bukoba na wadau wengine wakitoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao,
TRA Kagera waliunga mkono jitihada za kuwapa faraja watoto hao kwa kuwalisha wahudhuriaji wote zaidi ya 500 chakula.
Katika hatua nyingine, Mbunge Byabato amewaalika wana Bukoba wote katika Tamasha kubwa la Mkoa wa Kagera linalofanyika chini ya uanzilishi na usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi. Hajjat Fatma Mwassa kuanzia jumatatu ya tarehe 16/12/2024.
Wadau mbalimbali wamepongeza ubunifu, mafanikio na majitoleo hayo yaliyoratibiwa vema na Kamati ya Maandalizi na kuasa tamasha hilo liwe endelevu kwa ajili ya kuwaleta pamoja watu wote.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.23.jpeg597.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.31 (1).jpeg664.1 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.32.jpeg639.4 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.38.jpeg635.8 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.39.jpeg654.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.40.jpeg848.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.42.jpeg528.8 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.31.jpeg929.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.30.jpeg969.7 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.25 (1).jpeg964.2 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.25.jpeg718.1 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.24 (2).jpeg710.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.38 (1).jpeg412 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.36.jpeg558.5 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.24.jpeg531.4 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-12-15 at 16.48.24 (1).jpeg571.4 KB · Views: 2