Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
MBUNGE wa Jimbo la Chato mkoani Geita, Dk Medard Kalemani ameomba mamlaka zinazohusika kutoa ufafanuzi wa kile kilichopelekea ndege za abiria kuacha kutua uwanja wa ndege wa Chato.
Dk Kalemani ametoa malalamiko yake mbele ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Geita na kueleza hali hiyo imepelekea abiria wenye uhitaji wa usafiri wa haraka kupata usumbufu kwa kukosa huduma.
Amesema uhitaji wa ndege za abiria ni mkubwa kwani tangu uwanja wa ndege Chato uanze kutumika kuna mwitikio mkubwa wa abiria kutokana na miundombinu rafiki ya uwanja na uwepo wa abiria wanaoingia na kutoka Chato.
"Nilikuwa naomba kupitia kikao hiki, hebu tushawishi mgawanyo wa ndege chache zilizopo ziwe zinatua Chato hata kama ni mara moja kwa wiki, kwa sababu tuna kiwanja kizuri, kikubwa, kimejemgwa kwa fedha nyingi.
Pia soma
- Mashirika ya ndege yaukimbia uwanja wa ndege Chato. Hakuna ndege yoyote inayotua tena uwanjani hapo!