Mbunge Chato: Tunaomba ndege chache zilizopo ziwe zinatua Chato hata kama ni mara moja kwa wiki

Mbunge Chato: Tunaomba ndege chache zilizopo ziwe zinatua Chato hata kama ni mara moja kwa wiki

Uwanja wa Ndege chato ulikuwa unawasyani wa watu wanaoshuka 20 hadi 25 na waanopanda hivyohivyo,,kwa hiyo kusema uwanja hauna maana ni uwongo
Data za kupika chato nani apande ndege ? Mlipendelewa na aliyewapendele kafa na upendeleo wake
 
Mikoa ya Singida,Iringa ,Manyara nk.

Kinachotakiwa ni kuupa miundombinu inayohitajika kuhudumia biashara.

Sio lazima ilingane na Dar lakini taratiibu mda unavyoenda mambo yatakuwa Mazuri eg uwanja wa Ndege wa Dom unaweza kutumika kuleta Watalii wa hifadhi za Ruaha,Udzungwa,Manyara,Tarangile nk so utapata tuu international flights.

Kikubwa kulíko vyote ni kuimarisha biashara na uzalishaji
Mambo yatakuwa mazuri wakati Iringa kuna kiwanja kizuri tu na kinatoa huduma?

Mambo mazuri wakati Manyara imezungukwa na na KIA na Kiwanja cha Arusha ambapo kutoka pale ni karibu kwenda Babati?

Watu wenye akili za namna yako inawezekana ndo wapanga mipango huko Serikalini. Hamna akili kabisa.
 
Maamuzi mengi huwa kisiasa kuliko uhalisia


Kaangalieni Stendi zote zilizojengwa ni magofu, ukienda pale Dodoma hadi huruma.
Stendi inajengwa kilometa 10 toka katikati ya mji wakati mji wenyewe ukitembea 1km umeumaliza. Sema kwa miaka 20 ijayo stendi zitakuwa zimefikiwa na miji
 
Mambo yatakuwa mazuri wakati Iringa kuna kiwanja kizuri tu na kinatoa huduma?

Mambo mazuri wakati Manyara imezungukwa na na KIA na Kiwanja cha Arusha ambapo kutoka pale ni karibu kwenda Babati?

Watu wenye akili za namna yako inawezekana ndo wapanga mipango huko Serikalini. Hamna akili kabisa.
Kiwanja Cha Iringa sio Cha ndege kubwa
 
MBUNGE wa Jimbo la Chato mkoani Geita, Dk Medard Kalemani ameomba mamlaka zinazohusika kutoa ufafanuzi wa kile kilichopelekea ndege za abiria kuacha kutua uwanja wa ndege wa Chato.

Dk Kalemani ametoa malalamiko yake mbele ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Geita na kueleza hali hiyo imepelekea abiria wenye uhitaji wa usafiri wa haraka kupata usumbufu kwa kukosa huduma.

Amesema uhitaji wa ndege za abiria ni mkubwa kwani tangu uwanja wa ndege Chato uanze kutumika kuna mwitikio mkubwa wa abiria kutokana na miundombinu rafiki ya uwanja na uwepo wa abiria wanaoingia na kutoka Chato.

"Nilikuwa naomba kupitia kikao hiki, hebu tushawishi mgawanyo wa ndege chache zilizopo ziwe zinatua Chato hata kama ni mara moja kwa wiki, kwa sababu tuna kiwanja kizuri, kikubwa, kimejemgwa kwa fedha nyingi.

Pia soma
- Mashirika ya ndege yaukimbia uwanja wa ndege Chato. Hakuna ndege yoyote inayotua tena uwanjani hapo!
Watu wanaenda na upepo wa aliyepo juu.
Hivi yule mkuu wa TAKUKURU enzi za JPM alietaka kujenga nyumba kubwa chato hadi raisi akamwambia anajipendekeza,
Yuko wapi???
Nakumbuka alikuwa kanali wa jeshi
 
Kuna mambo mengi JPM alifanya yenye tija ila ule uwanja hapana. Alifosi. Hata ye nadhani alijua haikuwa sawa kujenga uwanja kule ila ndo hivo. Kufosi. Yaani hakuna hata basi la abiria lenye ruti ya Dar-Chato. Ila unaletewa uwanja wa ndege.

Ule uwanja ungejengwa geita mjini, ungekuwa na tija vizazi na vizazi.
 
Zitue tu kwa kumfurahisha marehehemu tahira aliyetumia mabilioni kujenga uwanja wa ndege sehemu ambayo si sahihi?
 
Uwanja wa Ndege chato ulikuwa unawasyani wa watu wanaoshuka 20 hadi 25 na waanopanda hivyohivyo,,kwa hiyo kusema uwanja hauna maana ni uwongo
Kwa idadi hiyo ya wasafiri, basi aerodrome ilikuwa inawatosha. Iweje unajenga Airport inayogharimu mabilioni ya pesa ilhali wasafiri hawafiki 30? Bado tuna matatizo ya kupanga na kuchagua kipi muhimu na sehemu ipi.
 
Stendi inajengwa kilometa 10 toka katikati ya mji wakati mji wenyewe ukitembea 1km umeumaliza. Sema kwa miaka 20 ijayo stendi zitakuwa zimefikiwa na miji
UONGO.
Msamvu iko mjini kabisa

Magufuli iko katikati kabisa ila kaangalie kule underground kuna maduka 100 hayana mteja hata 1
 
Kwa kuwa uwanja umekwishajengwa, itafutwe namna utumike, hata kama ni kwa kutumia Dash8. Kutokuutumia ni hasara zaidi.
wapewe wanajeshi tu, jamii ya huko haijiwezi kipesa
 
Dom ni Capital City no way lazima uwe na uwanja wa Kimataifa.

Hata Mikoa a jirani watatumia hasa Kwa cargo kikubwa ni kukuza shughuli za kiuchumi za watu na Mikoa ya jirani.

Pia wajenge Kumbi za Mikutano kubwa.
Sawa uwanja wa Kimataifa si lazima uwe mkubwa sana.
Sehemu kubwa ya hizi ndege za Kimataifa hubeba Wafanyabiashara
 
Aisee haswa, yaani utaona nyani ndio wamefanya makazi huko.
Inasikitisha sana akili za waafrika pindi wakiwa madarakani
Hebu fikiria huo mji wa Mobutu kwisha habari yake

Mwingine nae ni Bob Mugabe
Alituma jamaa yake mzungu kujenga Castle UK kwa thamani ya £41 million
Mpaka leo limetelekezwa na hakuna anaeishi na ni kubwa haswa

Sasa local residents wanalalamika kwa sababu pamekuwa sehemu ya kuuzia na kuvutia Unga na bangi kwa vijana
Hebu fikiria jengo limetupwa la mamilioni

Kuna watu wana laana mpaka walikoenda
Hili hapa jengo View attachment 3259879
Mkuu hiyo Hamilton Palace siyo mali ya Hayati Robert Mugabe.
Urafiki kati ya Mugabe na Nicholas van Hoogstraten mmiliki halali wa hiyo mali hakukupi uhalali wa kusema ni mali ya Mugabe.
Kwa jinsi Mugabe alivyo kuwa amewekewa vikwazo na UK enzi za uhai wake ingetaifishwa tu.
 
Hili liwe funzo kwa viongozi, wache ubinafsi. Eti chato int'l airport
 
Back
Top Bottom