Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Hakuwa na kitu cha kuzungumza mule ndani... C mnajua tena namna walivyoingizwa bungeni... Kudemka kunaendelea
 
Naona unaandika ukidhani kama kila mtu anajua nini kimetokea huko bunguni, eleza kiundani ikiwezekana weka na picha au video
 
Inasemekana dada alimsalimia habari za saizi dingi hakuitika alitaka aamkiwe shikamoo noma ikaanzia hapo, wengine wanasema dingi aliomba kazi akanyimwa ndio visa vikaanza
 
Wamevimbiwa na pesa za walipa kodi wa focus kwenye mambo yenye maslahi kwa taifa.
 
Ya msingi hawayafanyi kutwa kupoteza muda kwa vijembe na visasi. Nashauri wabunge walipwe mishahara usiozidi milioni 2 na allowance milioni 1 na wasilipwe kiinua mbongo, tuone kama atabaki mtu. Wabunge wetu wamekuwa mabwenyenye na miungu watu Inauma sana
 
Kumbe bunge letu halijawa huru hivi? Mbona mdada umependekeza tu.
 
Walishazoea kuwatoa nje wabunge wa CDM,sasa hivi wanatimuana wenyewe kwa wenyewe......"BUNGE LIMEPOTEZA DIRA HALINA MVUTO"
 
Hili ndilo analoweza mheshimiwa subwoofer ila kukumbatia Covid19 yeye haoni kama anavunja utaratibu kabisa 😅😅😅
 
Huyo Mbunge mwanaume yaani kazi yake ni kuangalia wanawake walivyovaa badala ya kujali maslahi ya jimbo lake?! Yaonekana hawajali raia jimboni, kwake ni posho na kuangalia kina mama walivyovaa, jamani hizi kura tuwapigie watu mahiri na wataotujali na kuleta maendeleo bungeni na siyo ujinga huo..
 
kule nyuma inawezekana mzigo unataka kuchana turubai
 
Wewe ndio utakua na matatizo ya akili
 
Haijakaa vizuri kabisa naona misimamo ya kidini inaletwa bungeni Islamic culture imepelekwa kwa ambaye sio muhusika eti avae nguo ndefu na baibui au ajitande, haipo sawa kabisa, pili alistahili kupewa onyo tu na sio kutolewa nje.
Sikubaliani na kitendo cha kutolewa nje huyo mbunge kwa sababu ya hilo vazi lake kwani kwenye picha inaonekana halina shida na wabunge kadhaa wanawake wamekua wakivaa mavazi kama yake

Lakini pia sikubaliani na wewe unapolaumu kwamba kuna mtu anataka kulazimisha Islamic culture, eti wabunge wanawake wajitande na wavae mabaibui! Hiyo tafsiri yako ni potofu na yenye kukera.

Si mbunge aliyetoa hoja(kwa maoni yangu kapotoka) wala spika aliyeamuru mama mbunge akabadili mavazi yake alizungumzia sababu za kidini. Tusiende huko. Hayo ni matatizo yao binafsi
 
Sidhani kama ni kanuni ndizo zilizomtoa. Baada ya hoja kutolewa Spika alitoa uamuzi wa kutoa bila kulisoma hilo vazi. Kwa maana hiyo alisikiliza upande moja... Uamuzi wake haukuwa wa busara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…