Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CONDESTER SICHALWE ASHIRIKI IBADA KANISA LA MORAVIAN KIJIJI NTINGA KATA YA MSANGANO
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe ameshiriki ibada katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Ntinga Kata ya Msangano ambapo amesisitiza watumishi na wachungaji kuwa na maombi ya kuombea Jimbo la Momba.
Katika ibada hiyo, Mhe. Condester Sichalwe akisoma Kitabu cha Yeremia. 33:1-3 amesema ipo haja ya kuomba kwa Mungu juu ya maendeleo ya Jimbo la Momba hususani katika Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya, Ulinzi na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ndani ya Jimbo la Momba
Mhe. Condester Sichalwe amechangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili (200,000) kwaajili ya ujenzi wa kuweka Malumalu (Tiles) kwenye sakafu ya Kanisa na kuahidi kuendelea kuwa na ushirikiano na viongozi wa dini zote katika Jimbo la Momba.