Mbunge Condester Sichalwe awasihi waumini Kanisa la Moravian kufanya maombi kwaajili ya Jimbo la Momba

Mbunge Condester Sichalwe awasihi waumini Kanisa la Moravian kufanya maombi kwaajili ya Jimbo la Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MBUNGE CONDESTER SICHALWE ASHIRIKI IBADA KANISA LA MORAVIAN KIJIJI NTINGA KATA YA MSANGANO

Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe ameshiriki ibada katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Ntinga Kata ya Msangano ambapo amesisitiza watumishi na wachungaji kuwa na maombi ya kuombea Jimbo la Momba.

Katika ibada hiyo, Mhe. Condester Sichalwe akisoma Kitabu cha Yeremia. 33:1-3 amesema ipo haja ya kuomba kwa Mungu juu ya maendeleo ya Jimbo la Momba hususani katika Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya, Ulinzi na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ndani ya Jimbo la Momba

Mhe. Condester Sichalwe amechangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili (200,000) kwaajili ya ujenzi wa kuweka Malumalu (Tiles) kwenye sakafu ya Kanisa na kuahidi kuendelea kuwa na ushirikiano na viongozi wa dini zote katika Jimbo la Momba.

Screenshot 2023-07-25 115139.png
 
Tumuombe Mungu ccm itoke madarakani, tupate katiba mpya tujenge nchi. MWANAKONDOO AMESHINDA, TUMFUATE
 
Mbunge mzima unachangia laki 2? Yafaa nini wakati tunajua unaenda kusuka pale dodoma kwa mkongomani kwa laki 7
 
Back
Top Bottom