Mbunge Daniel Sillo asema bila ya kuwa na Bandari imara Reli ya SGR haitakuwa na manufaa

Mbunge Daniel Sillo asema bila ya kuwa na Bandari imara Reli ya SGR haitakuwa na manufaa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Kamati ya bajeti na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daniel Sillo Julai 22, 2023 amesema ya kwamba wapo waliobeza filamu ya Royal Tour lakini leo watalii wameongezeka

Mhe. Daniel Sillo akasema hata swala la uwekezaji wa bandari lipo kwenye ilani na akawaomba watanzani kumuunga mkono Mhe. Rais Samia kwakuwa tunajenga reli ya kisasa bila kuwa na bandari imara reli haitakuwa na manufaa makubwa

Aidha, Ndugu Kinana Makamu Mwenyekiti CCM Taifa amemmwagia sifa Mhe. Daniel Sillo na kusema atashangaa mtu akichukua fomu ya kugombea ubunge 2025 zidi ya Mbunge wa Babati vijijini Mhe. Sillo kwa kazi kubwa anayoifanya japo hamzuii mtu kuchukua fomu maana ni demokrasia lakini atamshangaa na akawataka wananchi wamuulize huyo atakayechukua fomu ni kitu gani Mhe. Sillo hawezi kufanya yeye anaweza kufanya?

WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.23.jpeg
 
Royal tour imeleta watalii wapi?

Tanzania imekua ikipokea watalii miaka yote bila Royal tour.

Hakuna mtalii aliekuja sababu ya royal tour, hayupo.
 
Back
Top Bottom