Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Deo Sanga maarufu kama Jah People ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako, leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .

Chanzo: Mwananchi

FEE24A99-7195-43FF-8467-BF651436813C.jpeg

=====
Mbunge wa Makambako mkoani Njombe, Deo Sanga maarufu ‘Jah People’ amefunga ndoa na mkewe Suzana Kapasi leo Septemba 14, 2022 katika kanisa Katoliki Ilangamoto, Makambako Njombe.

Baada ya ndoa hiyo, hivi sasa sherehe ziliendelea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Amani ambapo Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Waziri wa Maliasili na Utali, Dk Pindi Chana.

Wengine ni wabunge mbalimbali akiwemo William Lukuvi (Isimani-Iringa), Festo Sanga (Makete) na Joseph Kamonga (Ludewa) pamoja na wananchi wa Mji wa Makambako.

Padri Ladislaus Mgaya wa Jimbo la Katoliki Njombe ndiye aliyewafungisha ndoa hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Deo Sanga , Maarufu kama Jah People , ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako , leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .

Chanzo : Mwananchi

Bado haijajulikana kama hii ni ndoa ya kwanza au la .
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa ni issue ya maisha binafsi ya watu, haki hiyo inabidi kuheshimiwa!.
P
Kwamba kuoa kwake ni siri au unataka kusema JF haturuhusiwi kuwaandika waliooa, tena waliooa hadharani? Huu ndio uanasheria uliosomea law school?

Pascal nani kakudanganya kwamba unao uwezo wa kutupangia cha kuandika?
 
Deo Sanga , Maarufu kama Jah People , ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako , leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .

Chanzo : Mwananchi

Bado haijajulikana kama hii ni ndoa ya kwanza au la .
Msaidieni na mwamba aige mfano wa Jah people afunge ndoa na Joyce siyo kumzalisha tuu.
 
Deo Sanga , Maarufu kama Jah People , ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako , leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .

Chanzo : Mwananchi

Bado haijajulikana kama hii ni ndoa ya kwanza au la .
Ukiishasema kafunga Ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki jua pasi na shaka hiyo ni aidha ni ndoa baada ya mkewe wa ndoa kufariki au ndoa yake ya kwanza. Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki huwezi kufunga ndoa kanisani kama una ndoa nyingine inayotambuliwa na Kanisa hilo.
 
Asante, japo mimi sikupishana na wewe.
 
Back
Top Bottom