Mbunge Deodatus Mwanyika: Serikali Iwalinde Wananchi Dhidi ya Wawekezaji Kwenye Ajira

Mbunge Deodatus Mwanyika: Serikali Iwalinde Wananchi Dhidi ya Wawekezaji Kwenye Ajira

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE DEODATUS MWANYIKA: SERIKALI IWALINDE WANANCHI DHIDI YA WAWEKEZAJI KWENYE AJIRA​

"Watu wa Jimbo la Njombe Mjini ni mashuhuda wa mafanikio makubwa ya kuwasogezea wananchi huduma mbalimbali ya kuboresha miundombinu, Madarasa, Usafiri wa Reli, Usafiri wa Anga. Tunamshukuru sana Mhe Rais Samia kwa yote ambayo yamefanyika" - Mhe. Deodatus Mwanyika, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini

"Shida kubwa ya Njombe ilikuwa ni upatikanaji wa Maji na hatukuwahi kuwa na uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Maji lakini ndani ya kipindi cha Miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt Samia tumekuwa na miradi mikubwa Minne ya Maji. Miwili imeshakamilika na inatoa Maji katika Mji wa Njombe"

"Wananchi wa Njombe wenye maji mengi lakini walikuwa katika mgao wa maji safi na salama. Lakini sasa wameanza kuonja matunda ya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maji. Tuna mradi wa Ijunilo wa Bilioni 3.9; Mradi wa Livingstone wa Bilioni 9.8; Mradi wa Miji 28 wa Bilioni 41. Jumla tuna Bilioni 67 katika Maji pekee yake"

"Vijiji vyote vya Njombe Mjini vina umeme na sasa tunakwenda kwenye vitongoji. Mji wa Njombe ni Mji na Vijiji, bado kwenye maeneo ya Mijini baadhi ya Mitaa hatuna umeme. Eneo la Mpumbwe n Ihanga halina umeme, naamini mpango unaokuja yatapata umeme"

"Ndani ya Mji wa Njombe tuna Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo Serikali iliingiza Shilingi Bilioni 27. Ina Vitanda 238 kati ya Vitanda 400 vinavyohitajika, Mama na mtoto ni Vitanda 100, Wakinamama 12 wanaweza kujifungua kwa wakati mmoja"

"Chuo Kikuu cha Dodoma kinafungua Tawi (Campus) Njombe Mji na Bilioni 18 zitawekezwa. Kiwanja cha Ndege Njombe kinakuja"

"Shida ya Njombe Mjini ni kutengeneza ajira, Njombe inategemea Kilimo kwa Asilimia 99 ambacho ni Mazao ya Chakula, Mazao ya Biashara na Mazao ya Misitu. Waziri Mkuu amekuja Njombe zaidi ya mara mbili na mara zote amekuwa akishughulika na changamoto ya uwekezaji"

"Sekta ya Uwekezaji kwenye Kilimo cha Chai ndiyo uwekezaji mkubwa Njombe lakini kuanzia Mwaka 2018 Sekta hii imedolola (Imekwama). Kukosekana kwa umakini katika kutafuta Wawekezaji kumekuwa na changamoto ya kukosekana kwa ajira maeneo ya Vijijini"

"Tunahitaji ajira, tunahitaji kodi na tunahitaji mazao ya kupeleka nje ya nchi tupate fedha za kigeni. Wawekezaji wa Chai wa kampuni ya DIEL umekuwa ni mwiba mkubwa sana kwa wananchi wa Njombe. Serikali iwe tayari kufanya maamuzi magumu kwa wawekezaji wa aina hii ambao wanapewa ardhi (Productive Assets) kama haitumiki kuzalisha ajira na kuzalisha bidhaa na kuleta fedha za kigeni maana yake hatuitumii kustawisha maisha ya wananchi wetu"

"Sekta ya Misitu ni suala la ajira, tuna kampuni kubwa ya Kibena ambayo ni mfano halisi wa Kampuni ya uwekezaji tunayotaka zije maeneo ya Njombe na maeneo mengine ya Tanzania. Ni kampuni ambayo inazalisha ajira, inaotesha Mazao (Plantations) na ikipewa ardhi inaitumia. Siku za karibuni tumeona makampuni mengi kutoka Asia yakija kuwekeza Sekta ya Misitu lakini kiuhalisia zinakuja kufilisi nchi ambao wanasafirisha malighafi ambapo nchi inapoteza ajira"

"Serikali ina jukumu la kuwalinda wananchi wake kuhakikisha wawekezaji hawapewi vibali vya kukata miti hovyo. Kuna mpango mkakati wa mwaka 2021 - 2030 wa kuongeza thamani kwenye Mazao ya Misitu, kuna GN ya 2023 namba 2.2.1 inayoruhusu Usafirishaji wa Malighafi za Misitu kwenda nje ya nchi. Tunaitaka Serikali kutumia GN kuzuia kutoa vibali kwa wawekezaji wa aina hii" - Mhe. Deodatus Mwanyika, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini
 

Attachments

  • DEO.mp4
    94.3 MB
  • nyikamkol.jpeg
    nyikamkol.jpeg
    341 KB · Views: 35
wengine wala hawajulikani ndio kwanzaaaaa tunaanza kuwasikia kisa uchaguzi umekaribia pigaaaaaaaaaaaaaa hao inzi, watanzania mnaonewa sana aisee.
 
Back
Top Bottom