PreGE2025 Mbunge Dkt. Charles Kimei azomewa Vunjo, Waziri Mchengerwa amtetea

PreGE2025 Mbunge Dkt. Charles Kimei azomewa Vunjo, Waziri Mchengerwa amtetea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Gazeti kazi yake ni kuhabarisha, na tukio limetokea kweli sasa wangeandika uongo kuwa wananchi wa Vunjo waliwapaka miguu waziri Mchengerwa na mbuge Kimei mafuta yenye manukato mazuri miguuni kwa furaha na nderemo huku wakibubujikwa na machozi ya furaha? Jamani waTanania tumekuwaje? Hatutaki viongozi wakosolewe au hata kukataliwa iwapo hawatekelezi majukumu yao ipasavyo au wanaposema uongo hadarani mchana kweupe?
Tutakua nchi ya aina gani? Rais Ruto jana kapigwa kiatu na magazeti yote ya Kenya yameandika TV na radio nazo zimetangaza sasa tatizo liko wapi waziri na mbunge kuzomewa kuandikwa na gazeti?
Akikujibu nipo pale nimekaa
 
Gazeti la mwananchi laiti ni sawa tu na BBC, Mwananchi ni ya Kenya hawana zuri na nchi yetu. Unavyoona BBC inavyoshughulikia Kenya ndivyo Mwananchi inavyoshughulikia nchi yetu. Hili gazeti ni mahasidi wanafurahia nchi yetu kuharibikiwa. Namkumbuka Magufuli ktk hili, hili ni gazeti la kufukuzwa. Shida ni waziri. Km mnaona vp kaeni pembeni tulinde nchi yetu.
Jamaa tangu atolewe ardhi morali imeisha kabisa. Ni kama sasa hivi anajilazimisha kufanya kazi.

Nyau de adriz
 
Kwa hali duni ya barabara ya Town - Kahe, sidhani kama kulikuwa na haja ya Dr. Kimei kufanya ziara Kahe.

Mzee Kimei aachane na siasa, akalee wajukuu; kwani sidhani kama kuna wa kumbeba zama hizi.
Njaa mbaya sana
 
Mwisho wa dynasty unakaribia, familia isome alama za nyakati
1746527955708.jpeg

Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa waziri wa TAMISEMI

02 May 2025

Mchengerwa Afunguka Uzoefu Wake Miaka 24 Kwenye Utumishi wa Umma, "Wanafikiri Huyu Mchengerwa Ameibuka Tu Jana"​


View: https://m.youtube.com/watch?v=QHxDnW9qWlA
 
Gazeti la mwananchi laiti ni sawa tu na BBC, Mwananchi ni ya Kenya hawana zuri na nchi yetu. Unavyoona BBC inavyoshughulikia Kenya ndivyo Mwananchi inavyoshughulikia nchi yetu. Hili gazeti ni mahasidi wanafurahia nchi yetu kuharibikiwa. Namkumbuka Magufuli ktk hili, hili ni gazeti la kufukuzwa. Shida ni waziri. Km mnaona vp kaeni pembeni tulinde nchi yetu.
Habari ni ya kweli au si ya kweli?
 
Kwa hali duni ya barabara ya Town - Kahe, sidhani kama kulikuwa na haja ya Dr. Kimei kufanya ziara Kahe.

Mzee Kimei aachane na siasa, akalee wajukuu; kwani sidhani kama kuna wa kumbeba zama hizi.
Sio hivyo tu, barabara za Uchira-Kirua Vunjo, barabara ya Himo-Mandaka na Kahe ni vumbi tupu na Mbunge yupo.
 
Kwa kile kinachoonekana mbunge wa Vunjo Dk Charles Kimei kuchokwa na wapiga kura wake baada ya kujikuta akipata wakati mgumu mbele ya waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa pale alipoanza kuzomewa na wananchi wake, hali iliyopelekea waziri Mchengerwa kuingilia kati na kuwasihi wananchi waache kumzomea mbunge wao kwani siyo mbunge muongeaji sana ila ni mbunge mchapakazi sana ndiyo maana amemleta waziri kuja kuzindua miradi.

Hata hivyo wananchi waliendelea kupinga kuwa mbunge Kimei siyo mchapakazi kwenye jimbo hilo.

----
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, amejikuta katikati ya zomea zomea katika Jimbo la Vunjo linaloongozwa na Dk Charles Kimei.

Hali hiyo ilijitokeza leo Mei 4,2025 kata ya Kahe wakati waziri huyo akizungumza na wananchi ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika jimbo hilo na kupokea taarifa ya kazi alizozifanya Mbunge kutoka kwa Katibu wake, Gulatone Masiga.

Hata hivyo, wakati akijibu maelezo ya Katibu huyo na kuelezea kuwa Mbunge huyo anafanya kazi kubwa, ndipo baadhi ya wananchi walionyesha kutokukubaliana naye na ndipo ilimlazimu kutumia dakika kadhaa kumwelezea Dk Kimei.

“Mbunge wenu anawasaidia sana. Inawezekana asijue kuongea sana. Inawezekana mbunge wenu asijue sana kuongea akawa mtendaji zaidi,” kauli hiyo ilijibiwa na sauti kutoka kwa baadhi ya wananchi kutokubaliana naye na wengine kuzomea.

“Sasa nyie mnafikiri nipo hapa kwa sababu gani. Naomba niwaulize swali. Si ni mbunge kanituma?Mnataka niondoke? Sasa kwanini mnamzomea mbunge?Kwa sababu mbunge kaniomba nije. Mmenisikia, mmenielewa sasa,”alisema Waziri.

“Wakati mwingine unawqeza ukawa na Mbunge asiwe mjanja mjanja sana lakini mkawa na Mbungeambaye anawasemea kero zenu na matatizo yenu. Kwa hiyo msiangalie upande mmoja tu,”alisisitiza Waziri Mchengerwa katika hotuba yake.

“Kwa sabau wazee wetu hawa wamefanya kazi sana kwenye taifa hili. Kwa hiyo endeleeni kuwa na imani na kwa sababu nimeona ninyi ni watu wenye subira. Kwani barabara hii si imedumu miaka mingi?”aliwauliza wananchi hao.

Waziri Mchengerwa alisema changamoto zilizoelezwa na Katibu wa Mbunge zimedumu kwa miaka mingi na wameendelea kuwa na Subira na kwa kuwa amefika hapo mwenyewe, basi changamoto zao zinakwenda kutatuliwa.

“Lakini hata haya tunayoyafanya wawakilishi wenu ndio wanaowasemea ndani ya Bunge na kuhangaika huku na kule kuhakikisha kwamba wameleta yale ambayo mngetamani kuyaona katika maeneo yenu,”alisema Waziri na kuongeza:-

“Msikate tamaa hata kidogo. Msibeze. Nawaambia wazi kabisa. Wakati fulani mnaweza kumtamani mtu fulani lakini yale ambayo mnataka yasifanikiwe. Lakini mkawa na mtu mtaratibu,anafuatilia kidogo kidogo bila kugombana na Serikali”

“Anapita huku waziri atakuja. Kwa hiyo niwaombe sana. Kwa namna ambavyo mmekuwa na subira, endeleeni kuwa na subira na sisi kama Serikali ya wanyonge tutahakikisha zile kero zetu tumezitatua na tumezimaliza,”alieleza Waziri.

Awali akizungumza kwa niaba ya Dk Kimei, Katibu wake alielezea mafanikio katika Jimbo hilo akitaja ujenzi wa kituo cha Afya kilichojengwa kwa Sh520 milioni na wana eneo ambalo wana uhitaji na zahanati katika kijiji cha Mwangaria.

“Kipo kwenye kata hii ambapo tumepewa Sh47 milioni kwa ajili ya kufanya jambo pale lakini kutokana na mgogoro wa Kanisa na wananchi, fedha zile zilirudi Serikalini. Kwa hiyo sasa tunakuomba wananchi wameshatenga eneo,”alisema.

“Pili tuna shule chakavu sana. Tuna shule ya msingi Oria pamoja na hiyo ya Mwangaria. Ni shule chakavu sana. Mheshimiwa waziri, mheshimiwa Mbunge alikuwa anaomba hayo,”alisema Katibu huyo na kuongeza kusema:-

“Kubwa zaidi ambalo limetuweka hapa ni barabara hii ambayo leo tunaitembelea. Barabara ya Mabogini-Kahe na Chekereni. Ni barabara ambayo wananchi wote walioko hapa watapata faraja na watafurahi sana kwa yale ambayo umetuletea”

Chanzo: Mwananchi
Huu mwaka tutaona na kusikia mengi
 
Eti niondoke? 😂 Hivi zama hizi unamtishia nani na kuondoka..zile zama za ndio mzee zimekufa na kuzikwa
 
Gazeti la mwananchi laiti ni sawa tu na BBC, Mwananchi ni ya Kenya hawana zuri na nchi yetu. Unavyoona BBC inavyoshughulikia Kenya ndivyo Mwananchi inavyoshughulikia nchi yetu. Hili gazeti ni mahasidi wanafurahia nchi yetu kuharibikiwa. Namkumbuka Magufuli ktk hili, hili ni gazeti la kufukuzwa. Shida ni waziri. Km mnaona vp kaeni pembeni tulinde nchi yetu.
Yaani kuficha ukhanithi ndio kilinda nchi?
 
Back
Top Bottom