Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE DKT. RITTA KABATI AYAPA NGUVU MASHINDANO YA SOKA YA UVCCM IRINGA, AAHIDI KUANZISHA "MAMA SAMIA CUP"
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Dkt. Ritta Kabati ameahidi kuanzisha mashindano yatakayojulikana kwa jina la Samia Cup kuenzi kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Kabati ameyasema hayo tarehe 24 Machi, 2023 katika uzinduzi wa mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya Soka yaliyoandaliwa na UVCCM Kata ya Kihesa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Amesema kuanzishwa kwa mashindano ya Kombe la Samia kutasaidia kutoa elimu kwa jamii katika nyanja mbalimbali, kutoa ajira kwa vijana kutokana na vipaji vyao na pia kuwaondoa vijana kushiriki masuala ya madawa ya kuleva.
Katika hatua nyingine Mhe. Kabati ametoa msaada wa shilingi laki nne kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano hayo yanayoelekea ukingoni.
Aidha, ametoa zawadi ya jezi na mpira kwa timu ya itakayofanikiwa kushinda nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo.