Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kutokana na kuenea kwa uvumi wa taarifa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwepo kwa maandamano awamu ya pili yanayotajwa kufanyika Desemba 9, 2025, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Paschal Chinyele amewataka viongozi wa mitaa kufuatilia wageni wanaoingia kwenye mitaa yao pamoja na kuwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwaripoti wageni wanaowatilia mashaka katika vituo vya polisi ili kuepusha taifa kuingia katika vurugu kama zilizotokea Oktoba 29, 2025.
Chinyele amebainisha hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Bonanza jijini Dodoma kwa lengo la kuimarisha usalama wa nchi kwa kulinda taifa lisiingie kwenye machafuko.
Chinyele amebainisha hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Bonanza jijini Dodoma kwa lengo la kuimarisha usalama wa nchi kwa kulinda taifa lisiingie kwenye machafuko.