Mbunge Edwar Lekaita aweka msisitizo maliasili na utalii kufanya kazi kwa karibu na WMA

Mbunge Edwar Lekaita aweka msisitizo maliasili na utalii kufanya kazi kwa karibu na WMA

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE EDWAR LEKAITA Aweka Msisitizo Maliasili na Utalii Kufanya Kazi kwa Karibu na WMA

Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoa wa Manyara, Mhe. Edward Ole Lekaita wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka mpya wq fedha 2024/2025 amesema WMA inasaidia wananchi kushirikishwa katika uhifadhi.

"Ilani ya CCM (uk.113) inasema, Kuimarisha mahusiano kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi. Huu ni msimamo (commitment) ya CCM. Naomba Waziri wa Maliasili na Utalii uwe mkali sana linapokuja jambo la mahusiano kati ya wananchi na watu wa hifadhi" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Ilani ya CCM inasema, Ili kuwa na uhifadhi endelevu ni lazima mjali Haki na Maslahi ya wananchi. Mali zao zilindwe, mashamba yao yalindwe, Mifugo yao ilindwe na maisha yao yalindwe, ukifanya hivi Waziri wa Maliasili na Utalii utakuwa mzuri sana"

"Waziri Mchengerwa alipokuwa Maliasili na Utalii alikuwa na kauli mbili nzuri; Wananchi Watanzania ni wahifadhi namba moja. Kazi zinazofanywa na Wahufadhi zitapimwa kwa kusikiliza wananchi watanzania wanataka nini"

"Utalii na Uhifadhi tunafikiri ni kuwa na Mbuga za Wanyama nyingi na mapori tengefu, Hapana, Siyo kweli! Nchi 10 Barani Afrika zenye maeneo ya hifadhi bado inasema Tanzania ina Mbuga 16 wakati tunajua tuna Mbuga za Wanyama 21 ambapo inafanya Tanzania iwe ya Tano badala ya kuwa ya pili ambapo ni Kenya, Tanzania na Zambia"

"Nchi zinazofanya vizuri ni Misri ambayo ina Watalii karibu Milioni 11 ambao wana Mbuga za Wanyama hazizidi Tano. Utalii tuufikirie kimapana zaidi. Ukitembelea Washington DC utalii watu wanakwenda African American Museums, Johnny Kennedy Memorial Centre, Martin Luther King Jr"

Nchi ya Morocco haina Mbuga nyingi sana za wanyama lakini watalii ni wengi kwasababu ya sababu nyingi zinazoleta watalii. Tunisia hawana Mbuga nyingi lakini watalii ni wengi sana. Tanzania asilimia 33 ya nchi ipo kwenye hifadhi"

"Waziri wa Maliasili na Utalii usikubali pendekezo lolote la namna ya kuongeza maeneo ya hifadhi kwasababu ongezeko la watu linaongezeka sana. Tuweke nguvu kwa haya tuliyonayo yasimamiwe vizuri na yalete mafanikio nchini"

"Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii mwaka 2023 na 2024 walisema na maazimio ya Bunge yalipitishwa fedha zinazodaiwa na WMA zirudi na Bunge lilisema, Tengenezeni mfumo utakaowezesha kila mdau apate fedha zake kwa wakati ili uhifadhi uendelee"

"WMA inafanya kazi kama Wizara ya Maliasili na Utalii inavyofanyakazi. Sioni sababu ya kugombania mipaka kwasababu wote tunafanya kazi moja ya kutunza mapori (Conservation). WMA ni nzuri kwasababu inafanya wananchi washiriki moja kwa moja kwenye uhifadhi"

"Nchi kama Namibia, Kenya, Botswana, Zimbabwe, South Africa, wote wanafanya kwa mfumo wa Module ya WMA. WMA zitauza vizuri Wizara ya Maliasili na Utalii maana inawezesha wananchi washiriki kwenye uhifadhi (Conservation)" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto.


 
Back
Top Bottom