Pre GE2025 Mbunge Edward Olelekaita: Hakuna tatizo kubadili jina la Tume ya Uchaguzi

Pre GE2025 Mbunge Edward Olelekaita: Hakuna tatizo kubadili jina la Tume ya Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Mbunge wa jimbo la Kiteto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Edward Olelekaita amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikubainisha Tume ya Uchaguzi iitwe jina gani, hivyo hakuna tatizo katika kubadili jina la sasa ambalo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Olelekaita ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa mwaka 2023.
 
Back
Top Bottom