Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. ENG. MWANAISHA ULENGE ATOA MCHANGO WAKE KATIKA MKUTANO WA 146 IPU
Mbunge wa Viti Maalum (Wanawake) Mkoa wa Tanga, Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge ashiriki katika Mkutano wa 146 kwenye Bunge la Dunia kupitia Jukwaa la Wabunge Vijana katika Umoja wa Mabunge ya Dunia.
Mnamo tarehe 14 Machi, 2023 Mhe. Ulenge alipata fursa ya kuchangia kwenye Bunge la Dunia kupitia jukwaa la Wabunge vijana katika Umoja wa mabunge ya dunia. Mada ya mkutano wa 146 wa IPU inahusu "Promoting peaceful coexistence and inclusive societies, fighting Intolerance".
Akichangia mada, Mhe. Ulenge alielezea hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania tangu Uhuru za kuwashirikisha vijana kwenye shughuli za maendeleo ya jamii huku wakiwezeshwa kulinda amani kwa miongozo na sheria mbalimbali zilizotungwa kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na utulivu.
Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani amewasilisha Hoja ya dharura kwa niaba ya kundi hilo kuchagiza kuundwa kwa Mfuko wa Maafa Duniani kwa ajili ya kusaidia Nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Machi 12, 2023 alihutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain.
Pia, Spika wa Bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Duarte Pacheco Jijini Manama nchini Bahrain wakati wa Mkutano wa 146 wa IPU.