Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE ESTHER MALLEKO AGAWA INCUBATOR KATA ZOTE ZA WILAYA YA ROMBO
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko ametembelea Wilaya ya Rombo na kuzungumza na wanawake wa UWT huku akiwakabidhi Mashine za Kutotolesha vifaranga vya kuku (Incubator) kwa lengo la kuwaepusha wanawake na mikopo inayoumiza (mikopo ya kausha damu)
"Leo nimekuja kutimiza ahadi yangu kwasababu mlinipa imani na mimi ninawalipa utendaji uliotukuka. Nimekuja kuwaletea mradi kwenye kila Kata katika Wilaya ya Rombo" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro
"Ninaamini hizi Incubator (Mashine za kutotolesha vifaranga) zikifika kwenye Kata zitaenda kukomesha mikopo ya kausha damu. Siasa ni uchumi na uchumi ni siasa. Tunaendelea kutafuta kura za Mama Samia wakati miradi inaendelea kukua"
"Mradi wa Incubator nataka uende kuwaunganisha akina Mama kwenye Kata na Matawi, Wanachama wa CCM, na wale wasio Wanachama wa CCM ili wajiunge na UWT kwa kuyaona matunda ya UWT"
"Mama Samia Suluhu Hassan hana deni na sisi, anatudai na tutamlipa yaliyotukuka. Miaka minne ametoa shilingi Trilioni 1.2 katika Mkoa wa Kilimanjaro. Mradi wa Maji Same - Korogwe umekamilika na Mama amemtua Mwanamke ndoo kichwani"