PreGE2025 Mbunge Francis Mtinga ataka wananchi wakatwe asilimia 10 ya kila vocha anayonunua kusaidia kwenye mfuko wa bima

PreGE2025 Mbunge Francis Mtinga ataka wananchi wakatwe asilimia 10 ya kila vocha anayonunua kusaidia kwenye mfuko wa bima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Naunga mkono hoja, ila napendekeza tukatwe 50%. Vocha ya 1000, wakate 500, kwa mwaka tutapata zaidi ya trillioni 15. Hii itakuza uchumi wa taifa.
 
Wakuu!

Hivi hawa wabunge wa kilala wa kiamka wanawaza tu wananchi wawe wanakatwa asilimia au tozo kuongezeka wao mbona awasemi wakatwe hizo posho zao au mishaara?

Mbunge Francis Mtinga amesema kila mwananchi wa Kitanzania anaye nunua vocha ya shilingi 1000 kwa siku akatwe asilimia 10 ambayo ni sawa na shilingi 100 ili ikasaidie kwenye mfuko wa bima kwa wato wasio na uwezo ili kila Mtanzania apate bima ya Taifa.

Amesema kutokana na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi amesema hiyo ni fursa kwa Watanzania ambao hawana bima ya afya.

Soma Pia: Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara

“Mimi napenda tukitumie chanzo hiki Watanzania mnielewe, tuchukulie kila Mtanzania anaponunua vocha ya Sh1,000 kwa siku atuchangie asilimia 10 tu ambayo ni Sh100 ambapo ukizidisha na laini zilizo hai milioni 90.4 nitapata kwa siku Sh9.4 bilioni nikipeleka kwa mwezi nitapata Sh271.2 bilioni na nikipeleka kwa mwaka nitapata S3.2 trilioni, zitakwenda kusaidia kwenye bima hiyo hata kwa wasiokuwa na uwezo

Hili ni wazo zuri Ila kama ikiwa hivyo ,huduma za afya kwa hospitali zote za serikali kuanzia zahanati mpaka Muhimbili ziwe ni BURE na BORA..
Hapo zamani sana enzi za utawala wa Nyerere wagonjwa hospitali walikua wanapatiwa matibabu,chakula na uniform za kuvaa bure,,,ukienda kumuona mgonjwa hospitali ulikua huendi na chochote.
 
Wameufilisi mfuko wa bima sasa wanataka mzigo waubebe wananchi. Wao si wanakula posho? Wakatwe posho zao ka laki kamoja tu kaende kwenye mfuko afu tuone.

Bila kusahau hizi chuma za LC400 wanazojinunulia wazi-downgrade kuwa prado kama wanauchungu na pesa.
 
Na wewe Mtinga onyesha uzalemdi kwa vitendo, mafao yako zaidi ya mil 500 unayokwenda kuyapata Bunge likivunjwa kesho kutwa yakatwe 30% kuchangia bima kwa wote.

Mpo wabunge zaidi ya 400 x 500m
30% × (400× 500m) = 60 bil

Hiyo hela inatosha kabisa kutunisha mfumo wa Bima nchini.
 
Naunga mkono hoja,masikini wanateseka sana kuhusu suala la matibabu
 
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche mishahara ya wabunge JPM aliacha 12.8M kwa mwezi lakini ikaongezwa hadi 19M. Yani mbunge wako analipwa milioni 20 kasoro moja. Pia John Heche alieleza kwamba posho zimeongezwa kutoka 360,000/= kwa siku hadi 620,000/= kwa siku. Hapo ni nje ya bima ya afya (daraja la kwanza) inayomuwezesha mbunge na familia yake kutibiwa hadi nje ya nchi. Ni nje ya milioni 90 anazopewa Mbunge kwa ajili ya gari. Ni nje ya 380M atakazopewa kama kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano.

Halafu katikati ya "ukwasi" huo anaibuka bwana Francis Mtinga "anayejiita" Mbunge wa Iramba, anataka watanzania wakatwe shilingi 100 kwenye simu kuchangia bajeti ya afya. Hivi amewaza kuna watanzania hata hiyo shilingi 100 kwao ni tabu? Sio ya kwenye simu, hata kuishika tu mkononi ni tabu.

Hivi anajua kuna akina mama kijijini wanatembea kilomita 10 au zaidi, kwenda porini kuokota kuni waje waziuze shilingi 500 wapate kula na watoto wao? Hivi amewaza kuna watu mwezi mzima simu zao hazijawahi kuwa hata na vocha ya kubeep, na wakitaka kuwasiliana na ndugu zao wanatuma please call me?

Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Badala ya wabunge kukatwa, wao wanataka wananchi wakatwe. What a greed? Extreme selfishness.

Mtanzania mmoja anashauri: njia sahihi ya kuchangia bajeti ya afya ni kushusha mishahara ya wabunge hadi 6M. Halafu hiyo 13M iende kuchangia afya. Tuna jumla ya wabunge 393 pale Dodoma. Kwahiyo serikali itakusanya Bilioni 5.1 kila mwezi kupitia makato hayo ya mishahara ya wabunge. Na pesa hizo ziende kusaidia afya ya watanzania.
 
Back
Top Bottom