Mbunge Fyandomo: Rais Samia Alitoa Ruzuku ya Mbolea Bei Ikashuka Kutoka 150,000 Mpaka 60,000 kwa Kilo Moja

Mbunge Fyandomo: Rais Samia Alitoa Ruzuku ya Mbolea Bei Ikashuka Kutoka 150,000 Mpaka 60,000 kwa Kilo Moja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE SUMA FYANDOMO: RAIS SAMIA ALITOA RUZUKU NA BEI YA MBOLEA IKASHUKA KUTOKA TSH. 150,000 MPAKA TSH. 60,000/KILO

"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Amir Jeshi Mkuu kwa kazi kubwa nzuri ambayo aliwaona wakulima maana walikuwa kwenye kipindi kigumu sana ambapo Mbolea ilikuwa na bei kubwa sana lakini Rais aliweza kutoa fedha za ruzuku kutoka Mfuko wa Mbolea wa Kilo 50 uliokuwa unauzwa kwa Tsh. 150,000 ukashuka bei mpaka Tsh. 60,000 mpaka Tsh. 70,000" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Bajeti aliyosoma Mhe. Hussein Bashe kuomba na ikapitishwa ya Tsh. Trilioni 1.2 ninaiunga mkono kwa asilimia Mia Moja. Nakupongeza Mhe. Hussein Bashe kwa kusimamia afya za watoto wetu kwa kufuatilia virutubisho vya Mchele ulioingizwa nchini kutoka Marekani" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Wilaya ya Rungwe, wananchi wengi wanategemea kilimo cha Chai, kuna Kiwanda cha Chai cha Chivante ambacho kimefungwa ambapo kuna wananchi wa Kayuki, Nsekela, Katonya, Ruwarisi, Ndende na Kiganga wananchi wote wana Chai za kutosha. Mhe. Hussein Bashe kaangalie kile Kiwanda wananchi wakichuma Chai wanaipeleka wapi?" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Kuna wakulima wa Chai waliopo Wilaya ya Rungwe ambao wanapeleka Chai kwenye Kiwanda cha Chai cha Katumba, wananchi wapo maeneo ya Rungwe, Kapugi, Masebe, Sekela, Mwakareli, Mamo, Lopa, Itete, Kimo, Suma na Nditu Wanafanya vizuri lakini wakulima hawapati fedha kwa wakati, wanazidishiwa sana muda" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Mwaka 2022 Serikali iliahidi Mufindi, Iringa kujenga Kiwanda cha kuchakata Maparachichi, eneo limepatikana na Kiwanda ni cha kusaidia wananchi wa Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Njombe, Mbeya, Iringa, Songwe. Tukuyu, Rungwe wamekazana sana kupanda Maparachichi baada ya kusikia kauli ya Serikali. Tunaomba Waziri utuambie ni lini Kiwanda kitaanza kujengwa" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Mbarali na Kyela zilitolewa Shilingi Bilioni 79 kwaajili ya Skimu za Umwagiliaji. Nakuomba Mhe. Hussein Bashe Mkoa wa Mbeya kuna Wilaya ya Mbeya DC, Busokelo, Chunya, Rungwe wanahitaji Skimu za Umwagiliaji. Wanawake na Vijana wanajituma kwenye mashamba maana ndiyo kazi yao kubwa" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-05-04 at 21.39.06.mp4
    14.9 MB
Kabla ya kupongeza tujiulize Wakati mama anaingia mbolea ilikuwa shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom