Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Wadau,
Nimeangalia kwenye YouTube, Bunge la Kenya na kuna Mbunge mmoja anaiitwa Duale ameishambulia Tanzania na serikali yetu kuwa tuna wabagua kwa nafasi za kazi kwa watu wao na biashara na pia amesema yule mbunge Jaguar alietoa kauli tata kuhusu kuondolewa kwa wafanyabiashara wa kitanzania nchini Kenya, yupo sahihi kulinda maslahi ya wakenya.
Ameishambulia sana serikali ya Rais Magufuli na Bunge la Tanzania.
Nadhani kuna kitu hakiko sawa kwa uapnde wa hawa wenzetu. Kuna chuki fulani dhidi ya watanzania.
My observation; naona tumekuwa pia tishio kwa wakenya kwenye ushindani kuanzia biashara mpaka kwenye ajira. Maana huyu mbunge kalalamika kuwa machungwa na kabichi wanazokula bungeni zinatoka Tanzania, masoko nchini Kenya yametekwa na watanzania. Heko watanzania wenzangu!
Ndiyo maana mimi nilikuwa na mashaka sana na hii East African Community, kwani tulikuwa nayo tangu zamani lakini kwa vile haikufurahisha matakwa yao wakati huo, wakaivunja na kupora mali zake karibu zote. Unapoiona KQ ikiwa juu ya airlines zote za Tanzania na Uganda leo ni kwa sababu walipora ndege zote zilizokuwa za EAA kasoro ile iliyotoroshwa na Capt Mapunda. Sasa hivi tunaelekea kurudia yale yale ila safari hii sijui watapora nini. Niliandika post moja ya kuonyesha mashaka yangu haya mwaka 2007 hapa, na miaka leo 12 bado mashaka hayo hayajanitoka.