Mbunge Garisa: Tanzania Walituchomea kuku,wakapiga mnada ng'ombe wetu

M
Kumbe hii vita ya Jaguar tuliianzisha wenyewe!! Sikiliza Majority Leader bungeni kenya leo.
Mpumbavu sana huyu,wasomili wenzake wamejazana kibao pale Isilii market nao ni foreigners kama Watz na Waganda
 
Mtapatapa sana yani ushawahi ona wapi eti mtanzania anashangilia watanzania wenzake wateseke ugenini eti kisa anamchukia magufuli? Halafu badae anataka kura zake?
Acha kuwa pimbi!Wapi nimeshangilia?Mnaambiwa chanzo cha yote haya ni matendo yenu ya hovyo alafu unasema ninashangilia!!!!

Na huyu mbungu kwenye hii clip wapi kasema watanzania wanyanyaswe?
 
Acha kuwa pimbi!Wapi nimeshangilia?Mnaambiwa chanzo cha yote haya ni matendo yenu ya hovyo alafu unasema ninashangilia!!!!
Kweli chadema hamna akili ya watanzania wanateseka wewe unaunga mkono? Nyie mataka madaraka kwa udi na uvumba hata kwa kumwaga damu za watanzania wenzenu?

Nabado 2020 inakuja watanzania tutawaonyesha kwamba tulifanya makosa kuwapa ubunge 2015 sasa lazima tuwafagie kwa fagio la chuma.
 
Mbunge wa Garisa mjini nchini Kenya Aden Duale amesema haungi matamshi ya Jaguar ila kuna mambo ya ovyo yanayofanywa na Rais Magufuli dhidi ya wakenya ambayo yanawakera sana

Amesema tangu Rais Magufuli aingie madarakani biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa ya ovyo sana,"walikamata kuku zetu wakachoma,wakakamata ng'ombe wetu wakapiga mnada,hivi vitendo si vya kiungwana kabisa" Alisema mbunge huyo ambaye ni mwenyekiti wa wabunge walio wengi bungeni

Aliongeza kusema ni haki serikali ilinde nafasi za kazi kwa wakenya ,kwani hata mkurugenzi wa Safaricom alizuiliwa kufanya kazi Vodacom Tanzania na serikali ya Tanzania kisa kulinda kazi za watanzania

My take,haya mambo yasipoingiliwa kideplomasia huenda kuna anguko lingine la jumuiya ya Afrika Mashariki linakuja

Source BBC
 
Wajkenya tunaishi nao vizuri sana hapa bongo wameoa kwetu, wamenunua viwanja na kujenga majumba, tunaishi nao kama ndugu, hapa kazini kwangu kuna Dada Wa Kikenya tunaye pamoja na vituko vyake vya kufumaniwa akipigwa P ofcn saaa tuna mchukulia tu.
Ni mjinga pekee asiyeona manufaa ya Tanzania kwa Kenya.
 
Wakenya walitufanya ndondocha ndo maana Mwalimu alipong’amua akafunga na mpaka. Kuna wakati sisi tulikuwa soko la bidhaa za Kenya. Kwa sasa wakenya wanaona tunavyochanja mbuga katika infrastracture, hivyo wanamchukia sana magufuli maana tunachanja mbuga. Wivu hata gharama za SGR, tulivyowapoka bomba la kutoka hoima unadhani waliPenda?
 

Tena kasema wazi haungi mkono matamshi ya Jaguar alafu wewe unaleta propaganda zako za kipuuzi mkidhani watanzania ni wajinga wasioweza kuchambua pumba na mchele!!
 
Kuna wajinga wa Lumumba ama hawana bundle kusikiliza clip nzima inasemaje au wameisikiliza na sasa wanaamua kupotosha alichosema kwa kuingiza propaganda zao za kipuuzi.

Hakuna mahali kaunga mkono matamshi ya Jaguar bali kaeleze uovu na sisi tuliofanya kwa wakenya.
 
Kwani hayo yote yalifanyika kisheria? Je kwasababu ya hayo mambo ambayo unahisi serikali ya tz ilikosea ndo ushadie watanzania wenzako wasio wanasiasa wapigwe nchini Kenya ambao wengi ni wachaga wenzenu?
Acha propaganda za kijinga!!Hiyo clip umeisikiliza?Jadili aliongea ya kumfukuza aliekuwa CEO wa voda,kuchoma vifaranga wa kenya,n.k.
 
Kwani hayo yote yalifanyika kisheria? Je kwasababu ya hayo mambo ambayo unahisi serikali ya tz ilikosea ndo ushadie watanzania wenzako wasio wanasiasa wapigwe nchini Kenya ambao wengi ni wachaga wenzenu?
Hayo ni yako wapi kasema unayosema?!

Kama hujasikiliza hiyo clip kaa kimya.
 
Huyo CEO wa bank akamatwe mara moja ahojiwe, anatuchonganisha
 
Hata mirungi yao pia tutaendelea kuikamata ni suala la kisheria wala siyo uungwana

Kama nchi yao wanaongoza kwa mujibu wa uungwana na siyo sheria ni wao

Mbona hakuna anayelalamika mtanzania kuhukumiwa miaka 99 jela kwa kuhusika na ugaidi Kenya?

Simply tunaheshimu sheria na taratibu zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…