Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Mkoani Mara, Boniphace Mwita Getere, akichangia hoja bungeni jana Oktoba 30, 2026,, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya nchi si ukosefu wa fedha au mipango mibaya, bali ni tatizo la usimamizi mbovu wa rasilimali na fedha za miradi ya maendeleo.
Akitoa mifano katika jimbo lake, Mbunge Getere amelalamikia kusuasua kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayochukua hadi miaka kumi kukamilika, huku wakandarasi wakipewa miradi mingi kwa pamoja na kushindwa kuitekeleza licha ya fedha kutolewa, hali inayowalazimu kuanza upya na kuongeza gharama za serikali.
Aidha, amegusia kero ya maji inayolikabili Jimbo la Bunda, akibaini kuwa vijiji 33 havina maji safi na salama na kutolea mfano Kata za Kitarale na Mihingo ambazo hazina hata kisima kimoja, huku akimwomba Waziri wa Maji kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ili wananchi waanze kupata huduma hiyo muhimu.