Mbunge Getere: Tatizo la nchi yetu ni usimamizi mbovu wa fedha, Kampuni moja inapewa barabara 10

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Your browser is not able to display this video.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini Mkoani Mara, Boniphace Mwita Getere, akichangia hoja bungeni jana Oktoba 30, 2026,, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayorudisha nyuma maendeleo ya nchi si ukosefu wa fedha au mipango mibaya, bali ni tatizo la usimamizi mbovu wa rasilimali na fedha za miradi ya maendeleo.

Akitoa mifano katika jimbo lake, Mbunge Getere amelalamikia kusuasua kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayochukua hadi miaka kumi kukamilika, huku wakandarasi wakipewa miradi mingi kwa pamoja na kushindwa kuitekeleza licha ya fedha kutolewa, hali inayowalazimu kuanza upya na kuongeza gharama za serikali.

Aidha, amegusia kero ya maji inayolikabili Jimbo la Bunda, akibaini kuwa vijiji 33 havina maji safi na salama na kutolea mfano Kata za Kitarale na Mihingo ambazo hazina hata kisima kimoja, huku akimwomba Waziri wa Maji kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ili wananchi waanze kupata huduma hiyo muhimu.
 
Ni ukweli usiopingika usimamizi wa rasilimali zote nchini pamoja na fedha ni mbovu sana....na hii tabia ishaota mizizi Kwa maana umeenda mbali zaidi,kipindi cha mwenda zake JPm tuliambiwa yamenunuliwa magari ya kuchimbia visima Kwa maana kila wilaya itapata gari moja, lkn la kushangaza ayo magari tuliyaona Kwa Taharifa ya habari na mwisho wa siku mpaka Leo hatuoni kinachofanyika kupitia ayo magari....
Wabunge wa ccm sometimes wanaongea km saa mbovu kwamba Kuna muda iyo saa inasema ukweli lkn Kuna muda inazengua majira yake....
 
Mbunge Boniface Mwita Getere, hicho ulicho kisema ni 100% correct, ila unashindwa kutamka wazi RUSHWA.
Wachina wanatoa rushwa kupata hizo kazi za ujenzi.
Siyo siri.
 
Mbunge Boniface Mwita Getere, hicho ulicho kisema ni 100% correct, ila unashindwa kutamka wazi RUSHWA.
Wachina wanatoa rushwa kupata hizo kazi za ujenzi.
Siyo siri.
Ni kweli jamaangu wachina washatushika pabaya sana, nakumbuka kipindi kile Barabara zinatengenezwa na makampuni ya kijapani, ya kiitaliano, na wajerumani Wakina(Astaldi, konoike, zakim, kojifar...mecco nk) Barabara ulikuwa unakuta zina ubora na zinakaa muda mrefu kutokuaribika...na Wala ukuwai kuisikia habari za 10% Kwa mkandarasi...lkn baada ya kuingia mchina ktk ardhi ya Tanganyika mambo yamebadilika....kabisa.
Barabara wanazojenga hazichukui muda zimeshachakaa unakuta Barabara Ina mwaka tu unakutana na mashimo makubwa km maandaki...Wachina washatujua kwaiyo wanaenda na jinsi tunavyoishi Barabara ya thamani ya 1BL Kwa kilomita moja unakuta msimamizi wa mradi anamwambia mchina kadiria iyo Barabara thamani yake isivuke 700ml pesa inayobakia tupia uko kwenye account Xx...mwisho wa siku Barabara inayotengenezwa ni chini ya kiwango na pesa washakula Wachina wa wakandarasi wazawa(wasimamizi wa mradi)
Na uwo ndo umekuwa mfumo hata Kwa wakandarasi wazawa km wakina nyazaroad, mambo ni Yale Yale...
 
Kuna wizi sana katika ujenzi wa barabara. Mawaziri wanahusika kuchukua 10%.

Kuna mfano barabara mbili kariakoo, za Lindi na Uhuru.
Lindi ilijengwa na mchina tena kwa fedha za World Bank, haikupita miaka mitatu barabara ilikufa kabisa.
Ile ya Uhuru ilijengwa na mkandarasi mzalendo, mpaka leo karibia miaka 10 inadunda.
RUSHWA toka viongozi wetu inaua nchi!
 
Ukiona hivyo ujue wizarani kumekufa, na hasa waziri husika kuwa na tamaa ya fisi.

Na hii ya contractor Moja kupewa favorite kuliko wengi, hii ni mbaya kwa ustawi wa jamii
 
Ukiona hivyo ujue wizarani kumekufa, na hasa waziri husika kuwa na tamaa ya fisi.

Na hii ya contractor Moja kupewa favorite kuliko wengi, hii ni mbaya kwa ustawi wa jamii
Wameamua kugawana keki wao tu Kwa staili wanayojua ...
 
Ukiona hivyo ujue wizarani kumekufa, na hasa waziri husika kuwa na tamaa ya fisi.

Na hii ya contractor Moja kupewa favorite kuliko wengi, hii ni mbaya kwa ustawi wa jamii
Harufu ya 10% haijifichi.
Wachina ndio zao.
Cha ajabu TAKUKURU wanataka waletewe mafaili ofisini badala ya kufanya sting operations.
Hizi dalili za rushwa huwezi kuepuka kuziona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…