Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE GHATI CHOMETE: CCM IMEJIPANGA VIZURI, LAZIMA ITASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Zephania Chomete, tarehe 26 Novemba 2024 ahitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwaombea kura wagombea wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini
Akizungumza na umati mkubwa wa Wananchi waliojitokeza kumpokea alipowasili Musoma Vijijini, Mhe. Ghati Chomete amewapongeza Wananchi hao kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa hiyo ni dalili nzuri sana kuwa Chama Cha Mapinduzi kinakubalika, kina nguvu, kimeenea na kitashinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Katika hotuba yake, Ghati Chomete ameelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara na Nchini kwa ujumla ambapo amesema miaka mitatu ya Rais Samia imeleta huduma karibu na wananchi tofauti na ilivyokuwa hapo awali hususan Elimu, Afya na Miundombinu.
Mhe. Ghati Chomete amewaomba akina Mama, akina Baba, Vijana, Wazee na watu wote waliofikia umri wa kupiga kura na waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi wanaotokana na CCM kwani kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mmoja na kutokupiga kura ni kutojitendea haki wewe binafsi.
Ghati Chomete amesema kuwa vyama vya upinzani bado havijakidhi vigezo vya kupewa hii nchi maana kama wao wenyewe ndani wameshindwa kujisimamia watawezaje kusimamia nchi kubwa kama hii ya Tanzania! Hivyo, wananchi wakiamini Chama Cha Mapinduzi maana kina ukomavu na uzoefu mzuri wa kuendelea kushika dola.
Mwisho, Ghati Chomete amewaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri anayoifanya nchini kote kwa kupeleka Maendeleo siyo tu Musoma Vijijini bali pia ndani ya Mkoa wa Mara na nchini kwa ujumla.