Mbunge Ibrahim Shayo apokwa Greda na Manispaa ya Moshi,ashindwa kukarabati barabara za pembezoni,Greda lapelekwa mradi wa TACTIC

Mbunge Ibrahim Shayo apokwa Greda na Manispaa ya Moshi,ashindwa kukarabati barabara za pembezoni,Greda lapelekwa mradi wa TACTIC

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
IMG_20260925_113107_662.jpg


Kuna sintofahamu imeibuka baada ya Greda la Manispaa ya Moshi alilokuwa akilitumia mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Ibrahim Mohamed Shayo kukarabati barabara za pembezoni mwa jimbo lake kudaiwa kuwa bovu hali ambayo imemfanya mbunge huyo kushindwa kuendelea na ukarabrati wa barabara hizo .

Habari ambazo tumezipata ni kwamba mbunge huyo alilitumia Greda hilo kwa siku Saba tu kukarabati barabara kwenye Kata tatu tu kati ya Kata 21 zinazounda jimbo la Moshi mjini

Wakati Greda Hilo lenye namba za usajili MS 11454 likidaiwa kuwa ni buvo kamaera yetu imefanikiwa kulinasa likitekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwenye mradi mkubwa wa uhoreshaji wa miundombinu ya barabara na mifereji ya mvua wa TACTIC eneo la daraja la Otieno Kata ya Msaranga.

IMG-20260925-WA0031.jpg


Mradi huo ambao hata hivyo ujenzi wake umekuwa wa kusuasua unatekelezwa kwenye Kata nane kati ya 21 za Manispaa ya moshi wenye urefu wa Kilometa 13.

Akiwa mjini moshi hivi karibuni ,Waziri wa Afya Mohamed Nchengerwa alikemea vikali hatua ya uongozi wa Manispaa ya Moshi kumnyima Greda hilo mbunge shayo na siku chache baadae Manispaa ilimkabidhi greda hilo .

Baadhi ya madiwani waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao wamekielezea kitendo hicho kama dharau kwa Waziri na kwa wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara kwenye maeneo yao.

IMG-20260925-WA0016.jpg


Waziri Chengerwa ambaye alionekana kukerwa na msuguano huo alisema mbunge kama mwakirishi wa wananchi anaowajibu wa kuwatumikia wananchi

Mradi huo wa TACTIC unafadhiliwa na serikali kuu kwa mkopo wa Benki ya dunia wenyewe thamani ya doal za marekani milioni 410 sawa na Bilioni 22.9 na unatekelezwa na mkandarasi M/S Hari Singh and Sons kwa ushirikiano na kampuni ya Peritus Exim Private Ltd .

Hapo chini tunakuwekea video ya waziri Nchengerwa iliyosamabzwa na Afya News akikekemea msuguano huo na kuhoji "mkurugenzi unauhakika utakaa miaka mitano hapa?,"

 

Attachments

  • IMG-20260925-WA0047.jpg
    IMG-20260925-WA0047.jpg
    115.2 KB · Views: 8
  • IMG-20260925-WA0025.jpg
    IMG-20260925-WA0025.jpg
    97.1 KB · Views: 8
  • IMG-20260725-WA0340.jpg
    IMG-20260725-WA0340.jpg
    323.9 KB · Views: 12
Back
Top Bottom