Pre GE2025 Mbunge Jafari Chege amesema kiongozi mzuri ni yule anayeweka alama kwa wananchi

Pre GE2025 Mbunge Jafari Chege amesema kiongozi mzuri ni yule anayeweka alama kwa wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

GMu9jj2XQAALKmt.jpg

Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura Chege amesema ndani ya siku 30 Serikali itaanza matengenezo ya Barabara ya Nyarombo - Siko - Busanga ya Kilometa 8 baada ya Serilkali kutenga Milioni 90 kwaajili ya Matengenezo hayo.

Mhe. Jafari Chege amesisitiza wananchi wa Kijiji cha Busanga Kata ya Nyamutinga kuanzisha ujenzi wa Sekondari mpya ili kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea takribani Kilometa 10 ambapo ameahidi kutoa mifuko 100 baada ya kuanzisha ujenzi huo.

GMu-tQmXsAAyBQu.jpg

Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura Chege ametumia fursa hiyo kusikiliza changamoto za wananchi wa kijiji cha Busanga Kata ya Nyamutinga Wilaya ya Rorya ambao wamefunguka mambo mbalimbali na kumuomba Mbunge wao wa Rorya kuyafanyia kazi.

Wananchi wa kitongoji cha Siko kijiji cha Busanga Kata ya Nyamutinga Wilaya ya Rorya Mkoani Mara wameiomba Serikali kutatua changamoto ya Miundombinu ya Barabara, Umeme, Maji na Miundombinu ya Shule ya Msingi Siko.

IMG_20240504_163026.jpg
 

Attachments

  • y2mate.com - MBUNGE JAFARI KIONGOZI MZURI NI YULE ANAYEWEKA ALAMA KWA WANANCHI_360p.mp4
    31.2 MB
  • GMu9jpCWQAAWGIq.jpg
    GMu9jpCWQAAWGIq.jpg
    477.4 KB · Views: 3
  • GMvr9emWUAAn-El.jpg
    GMvr9emWUAAn-El.jpg
    552.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom