Mbunge Jaguar kujipeleka polisi - hivi mbona Watanzania ndio wamecharuka sana japo wengine walitajwa

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Edit: Habari za hivi punde, mbunge Jaguar amekamatwa na polisi https://www.kenyans.co.ke/news/41074-jaguar-arrested-outside-parliament-buildings
-----------------
Muda wowote mbunge Jaguar atajipeleka kwenye kituo cha polisi baada ya uchunguzi kuanza kufanywa ili kubaini sheria ipi alivunja alipotoa matamko ya kuwatishia wageni. Kwa kweli alichokifanya ni mbaya zaidi na anafaa achukuliwe hatua za kisheria, ila nauliza tu, mbona humo alitaja raia wa kutokea mataifa mengine wakiwemo Waganda, lakini wote hao wapo kimya ila kwa Tanzania jana bunge halikua linakalika, mpaka hata waziri mkuu alilazimika kutoa tamko.

Siku zote nilijua Watanzania hawana haja ya kuja Kenya, na kwamba wao husema kwao huko ni nchi ya asali na maziwa. Iweje siku Watanzania walichinjwa Afrika Kusini walipiga kimya, Watanzania mamia wamefurushwa na kuteswa Msumbij hapo jirani wao, pia kimyaaa.... lakini hapa mbunge kwa kunywa gongo/chang'aa yake akabwatuka na kutaja taja wageni wa mataifa tofauti, lakini imeongelewa Bongo yote wamelia sana.

Hii iwe funzo kwa jirani zetu mnaopenda kiburi, sote ni ndugu, tunategemeana kwa njia moja au nyingine, mna desturi ya kuonyesha chuki dhidi ya Wakenya huko kwenu mkijiona kama kwamba nyie ndio kila kitu, lakini mwenye akili kati yenu akaombe takwimu za uhamiaji aone Watanzania wangapi wanakesha wakija huku Kenya.
-------------------------

Developing: Starehe MP Jaguar to present himself at parliament police station over xenophobic remarks. More details to follow on #TheDailyBrief.
D9-NZffX4AAlG5Q.png

Wengine wetu wazalendo lazima tumsapoti huyu mbunge wetu jamani!! watz pia walifurahikia hatua za jiwe kupiga mnada ngombe za wa maasai kule loitoktok na namanga, bila kusahau uchomwaji wa vifaranga! nyuzi za kusifia hizo hatua zilijaa sana humu....ila aisee wachaga wamejaa sana huko gikomba, watupishe na sisi wazawa tumiliki hizi biashara zao mazee...si jiwe anasema uchumi unapaa kule tz, warudi zao tu huko haumizwi mtu
 
Uchokozi ndio hatupendagi Chief!

Watanzania wamefukuzwa bila huruma na wengine kuteswa na kunyang'anywa mali yao kule Msumbiji, ambayo jirani wenu hapo, pia ni nchi ambayo mlimwaga sana damu yenu ili kusaidia kuikomboa, mbona hamkusema kitu, mliufyata...sasa hapa mbunge ametafuna mirungi na kufyatuka maneno dhidi ya raia wa nchi kadhaa, lakini nyie ndio mumelia sana ilhali wenzenu wote kimyaa

-------

Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

https://www.bbc.com/swahili/habari-38981965
 
Tatizo serikali yenu ilikalia kimya kwanza kusikiliza mshindo. Afu Tanzania hatupendi ubaguzi
 
Msumbiji/Malawi hatutangamani nao sana, tena hawapo EAC, pia wao hawana 'nyodo' kama nyie Wakenya! Mnajiona mko juu sana kila sekta wakati hamna kitu! na ndio maana nyie ndio MAHASIMU wetu wakubwa zaidi Duniani!
 
Nyie watu tunawafundisha kuacha tabia yenu ya ubaguzi inabidi mshukuru kwa kuwa na jirani anayewapigania muwe wastaarabu Kama Tz.
 
Wengine wetu wazalendo lazima tumsapoti huyu mbunge wetu jamani!! watz pia walifurahikia hatua za jiwe kupiga mnada ngombe za wa maasai kule loitoktok na namanga, bila kusahau uchomwaji wa vifaranga! nyuzi za kusifia hizo hatua zilijaa sana humu....ila aisee wachaga wamejaa sana huko gikomba, watupishe na sisi wazawa tumiliki hizi biashara zao mazee...si jiwe anasema uchumi unapaa kule tz, warudi zao tu huko haumizwi mtu
Kenyans we can be all things,but not this one.We don't attack neighbours simply because they are here to look for a living.We haven't reached that level....So I don't support the utterances by that stupid MP!
 
jiwe alfurahia kupiga mnada ngombe kule namanga pamoja vifaranga! nasema wachagga wa gikomba walambwe tu nao waliskie joto la jiwe..

Chicks+pic.jpg
images.jpg
maxresdefault.jpg
 
Watanzania wamefukuzwa bila huruma na wengine kuteswa na kunyang'anywa mali yao kule Msumbiji, ambayo jirani wenu hapo, pia ni nchi ambayo mlimwaga sana damu yenu ili kusaidia kuikomboa, mbona hamkusema kitu, mliufyata...sasa hapa mbunge ametafuna mirungi na kufyatuka maneno dhidi ya raia wa nchi kadhaa, lakini nyie ndio mumelia sana ilhali wenzenu wote kimyaa

-------

Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

https://www.bbc.com/swahili/habari-38981965

Juzi Museveni alitangaza kupiga risasi Mfugaji yeyote wa Kenya atakaevuka boda, Wakenya kimyaa, sipati picha kama Jiwe angetoa hilo Tamko.
Tanzania ilipiga mnada Ng’ombe wengi wa Uganda, Kenya na Rwanda, Ng’ombe wa Rwanda na Uganda ndio walikuwa wengi sana ajabu UG na RW walijua wamekosea wakakaa zao Kinya, ila vile Vilio wakenya walilia nahisi hata mzee Kenyatta alisikia huko ahera.
 
Sisi tulipiga kelele maana mlionyesha wazi chuki yenu dhidi ya chochote cha Kenya ni sera ya kiserikali, matukio ya kudhihrisha chuki yalfanywa na serikali na pia hata rais wenu akaweka wazi kwamba huo ndio msimamo wa Tanzania.
Lakini kwa hili la Jaguar ambalo limewanyima usingizi hadi bungeni likawa mjadala uliomhusisha waziri mkuu, sio sera ya serikali yetu, ni mbunge kalewa mirungi na kufyatuka.

Nchi yetu haijatokea hata sku moja ikawabagua Watanzania wala kuonyesha chuki zozote dhidi yao, wapo wamewekeza huku na serikali yetu imefutilia mbali baadhi ya sheria ili kuwarahisishia wageni wengi waje kuwekeza, hivyo kuna tofauti kubwa sana baina yetu na nyie.
 
Msumbiji/Malawi hatutangamani nao sana, tena hawapo EAC, pia wao hawana 'nyodo' kama nyie Wakenya! Mnajiona mko juu sana kila sekta wakati hamna kitu! na ndio maana nyie ndio MAHASIMU wetu wakubwa zaidi Duniani!

Hao Msumbiji mko nao kwenye SADC ambayo huwa mnasema ndio ndugu wenu zaidi, ila huwa hawawataki huko, sisi huku tumeruhusu hadi omba omba wenu wamejaa pembeni mwa barabara zetu na hakuna anayeulizwa kitu. Tazama hii video

Sisi tulipiga kelele maana mlionyesha wazi chuki yenu dhidi ya chochote cha Kenya ni sera ya kiserikali, matukio ya kudhihrisha chuki yalfanywa na serikali na pia hata rais wenu akaweka wazi kwamba huo ndio msimamo wa Tanzania.
Lakini kwa hili la Jaguar ambalo limewanyima usingizi hadi bungeni likawa mjadala uliomhusisha waziri mkuu, sio sera ya serikali yetu, ni mbunge kalewa mirungi na kufyatuka.

Nchi yetu haijatokea hata sku moja ikawabagua Watanzania wala kuonyesha chuki zozote dhidi yao, wapo wamewekeza huku na serikali yetu imefutilia mbali baadhi ya sheria ili kuwarahisisha wageni wengi waje kuwekeza, hivyo kuna tofauti kubwa sana baina yetu na nyie.

Mnahisi hivyo sababu Mko emotional sana, na mkiwagusa hao watz huko ndio mtaelewa vizuri somo.
 
na w
Watanzania wamefukuzwa bila huruma na wengine kuteswa na kunyang'anywa mali yao kule Msumbiji, ambayo jirani wenu hapo, pia ni nchi ambayo mlimwaga sana damu yenu ili kusaidia kuikomboa, mbona hamkusema kitu, mliufyata...sasa hapa mbunge ametafuna mirungi na kufyatuka maneno dhidi ya raia wa nchi kadhaa, lakini nyie ndio mumelia sana ilhali wenzenu wote kimyaa

-------

Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

https://www.bbc.com/swahili/habari-38981965
Na wewe sijui umeishakula mirungi? kinachoongelewa hapa ni raia walioingia nchi jirani with permit. Hawa ndio unaweza kuwatetea, lakini wanaoingia nchi jirani bila permit, hawa linalowakuta ni wao watajijua.
 
Mnahisi hivyo sababu Mko emotional sana, na mkiwagusa hao watz huko ndio mtaelewa vizuri somo.

Watanzania wameguswa kwingi na majirani zenu lakini mpo kimyaa kwa uwoga, juzi hapa Wanyarwanda wamewaua wavuvi wa Kitanzania, mbona hamkuwapa somo, Watanzania wamenyanganywa mali na kufukuzwa Msumbiji kimyaaa, acheni hicho kiburi, mfahamu ukanda wote huu sisi pekee yetu ndio tunawavumilia hadi omba omba wenu wamejazana huku. Tazama hii video ya mlichofanywa na Wanyarwanda

Msumbiji/Malawi hatutangamani nao sana, tena hawapo EAC, pia wao hawana 'nyodo' kama nyie Wakenya! Mnajiona mko juu sana kila sekta wakati hamna kitu! na ndio maana nyie ndio MAHASIMU wetu wakubwa zaidi Duniani!
Subiri mechi ya kesho
 
Watanzania wamefukuzwa bila huruma na wengine kuteswa na kunyang'anywa mali yao kule Msumbiji, ambayo jirani wenu hapo, pia ni nchi ambayo mlimwaga sana damu yenu ili kusaidia kuikomboa, mbona hamkusema kitu, mliufyata...sasa hapa mbunge ametafuna mirungi na kufyatuka maneno dhidi ya raia wa nchi kadhaa, lakini nyie ndio mumelia sana ilhali wenzenu wote kimyaa

-------

Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

https://www.bbc.com/swahili/habari-38981965
Kama walikua wanakaa bila vibali je
 
Back
Top Bottom