Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE JANEJELLY NTATE AWAOMBA WANANCHI KUWA WALINZI WA MIRADI YA MAJI INAYOZINDULIWA KIPINDI HIKI CHA MBIO ZA MWENGE
Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate katika sherehe za Mbio za Mwenge Temeke, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maslahi ya watumishi, kuleta fedha za kutosha na kufanya watumishi sasa kufanyakazi kwa weledi na uadilifu.
"Wasimamizi wa miradi hii ni watumishi ambapo tumeona hatimaye miradi yote imekubaliwa kufunguliwa na mingine kuwekewa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa" - Mhe. Janejelly James Ntate
Mhe. Janejelly James Ntate aliwaasa watumishi kuwa wabadirike sasa na waelewe wao ndio walinzi wakuu wa rasilimali fedha, ambayo Wabunge wamekuwa wakiomba Bungeni na Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayeongoza Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuleta fedha hizo.
Mhe. Janejelly James Ntate Aliwaomba wananchi kuwa walinzi wakuu wa miradi iliyozinduliwa hasa miradi ya Maji kwani hizo ni Kodi zao.