Mbunge Juliana Masaburi Ahoji Utekelezaji wa Mradi wa REA III Mkoa wa Mara

Mbunge Juliana Masaburi Ahoji Utekelezaji wa Mradi wa REA III Mkoa wa Mara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi katika kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni Jijini Dodoma amehoji Wizara ya Nishati kuhusu utekelezaji wa Miradi ya REA III awamu ya Pili Katika Mkoa wa Mara

Maswali yote yalijibiwa na Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato na kuelezea mipango na mikakati mbalimbali ya Wizara kuisimamia REA ili kufikisha Umeme kwenye kila Kitongoji

"Je, Ni lini mradi wa Kilomita mbili (02) za nyongeza katika Mradi wa REA III awamu ya pili utaanza kutekelezwa katika Mkoa mzima wa Mara?" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Tunatarajia Ijumaa ya Wiki hii REA watakaa na wakandarasi, wameshapewa idhini ya kuendelea na maeneo ya kutekeleza kilomita mbili, wakishasaini Mikataba mwishoni mwa Wiki hii tunatarajia mwanzoni mwa mwezi unaokuja kazi itaanza na mwa kuwa kazi ni ndogo tunatarajia itakamilika pamoja na kazi kubwa mwezi disemba mwaka huu kwasababu ni kupeleka Line ndogo za kuwasha Umeme katika Vijiji vyote ambavyo vilikuwa katika REA III awamu ya pili kwa maana ya kuongeza kilomita mbili kwa kila Kitongoji" - Mhe. Wakili Stephen Byabato, Naibu Waziri Nishati

maxresdefaultWQA.jpg
 
Ccm majina ni yaleyale, alianza babu mpaka Mjukuu.

Utashangaa jitu linaitwa Mashambwa linashabikia Ccm, matokeo yake linabaki kuwa Karai tu
 
Back
Top Bottom