Mbunge Juma Usonge awataka wazazi kushirikiana na Walimu kuwahimiza wanafunzi kusoma kwa Bidii

Mbunge Juma Usonge awataka wazazi kushirikiana na Walimu kuwahimiza wanafunzi kusoma kwa Bidii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Chaani Mhe. Juma Usonge amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanakijiji kwenye kikao cha kuratibu shughuli ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa Skuli ya Sekondari ya Pwani Mchangani kwenye ukumbi wa Skuli ya Sekondari Pwani Mchangani iliyopo Wiliya ya Kaskazin A Unguja.

Mhe. Juma Usonge amesema hajaridhishwa na baadhi ya matokeo ya ufaulu wa wanafunzi kidato cha nne mwaka 2022 na ameitaka Kamati ya Skuli ,Walimu na Wazazi kwa pamoja kushirikiana kuandaa mipango madhubuti ya kitaaluma ili kuweza kuwahamasisha na kuwafundisha wanafunzi ili kuweza kupata matokea mazuri na kuwawezesha wanafunzi kufika malengo yao.

Mhe. Juma Usonge amesema atahakikisha changamoto zilizopo anashirikiana wa Walimu, Wataalam mbalimbali na Jamii kwa ujumla ili kuwawezesha Wanafunzi wanafaulu vizuri kwenye masomo yao.

Kwa upande wa Walimu wamesema tatizo la uhaba wa Walimu katika Skuli hiyo ni changamoto kubwa iliyopeleka kufanya vibaya katika ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2022 na wameiomba mamlaka husika kuwaongezea Walimu ili kuzidisha nguvu katika ufundishaji.

Nao Wanakijiji waliohudhuria katika kikao hicho wamempongeza Mbunge na Kamati kwa kuleta wazo zuri la kuandimisha miaka 50 tangu kuanzishwa Skuli hiyo kwani Maadhimisho hayo yatakuwa na Tija ya kuleta ushirikiano na mshikanamo na wakuwasaidia vijana kujitambua na kujitathimini zaidi katika sula la elimu.

WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.40.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.39(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.38.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.37(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-26 at 19.09.36.jpeg
 
Ye kasoma nini? Angekua na akili asingepitisha DP World!
 
Back
Top Bottom