Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti, ametoa wito kwa Serikali kuongeza msisitizo katika sekta ya kilimo kupitia programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) kama suluhisho la kudumu la ajira kwa vijana na kukuza pato la taifa.
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Vijana bungeni, leo Aprili 20, 2026 Kafiti amesisitiza kuwa vijana ndio tegemeo kuu la taifa, hivyo kuna haja ya kuwapa kipaumbele katika mipango ya maendeleo.
Soma: Wizara ya Vijana yaomba Tsh. Bilioni 35.9 kuimarisha Maendeleo ya Vijana 2026/27
"Eneo la kilimo kupitia BBT tuendelee kuweka msisitizo. Vijana wengi watakwenda kuajiriwa hapa. Tunafahamu tuna vijana wanatoka SUA. Ni ajabu kumwona graduate wa SUA anakwenda kutafuta kazi wakati kuna nguvu kazi serikali inaweza ikatoa mitaji vijana hawa wakaenda kujiajiri."
"Tuna vijana wanaomaliza mikataba JKT. Wakimaliza wanarudi mtaani. Kwa nini tusiwaanzishie mashamba ya wao kujiajiri na kuweza kuchangia pato la taifa? Kwa hiyo tunafahamu tuna uhaba wa sukari. Vijana waende tuwaanzishie mashamba, mitaji waende wakalime."