Mbunge Kaliua Ampongeza Waziri Mkuu Juu ya Maelekezo kwa Jeshi la Polisi Kutatua Migogoro ya kwenye Hifadhi

Mbunge Kaliua Ampongeza Waziri Mkuu Juu ya Maelekezo kwa Jeshi la Polisi Kutatua Migogoro ya kwenye Hifadhi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE KALIUA, MHE. ALOYCE KWEZI AMPONGEZA WAZIRI MKUU KWA MAELEKEZO ALIYOYATOA BUNGENI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KWENYE HIFADHI

Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Aloyce Andrew Kwezi amempongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa hotuba nzuri aliyoitoa leo Bungeni Jijini Dodoma ya kulitaka jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa wananchi walionyang'anywa ardhi yao.

WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim Majaliwa amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza matukio yote yaliyotolewa taarifa kuhusu kuteswa, kuumizwa na kuuawa kwa baadhi ya Wananchi waliotuhumiwa kuingia ndani ya hifadhi na watakaobainika wachukuliwe hatua stahiki.

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi (Aprili 27, 2023) Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kusimamia masuala ya uhifadhi.

Amesema kuwa Operesheni zote katika maeneo ya hifadhi zifanyike baada ya wananchi wa maeneo husika kushirikishwa na kupewa taarifa za kutosha na sio kuvizia “Kufanya hivyo kutaiwezesha Serikali kuendelea kuimarisha uhifadhi endelevu kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wahifadhi wahakikishe wanazuia mapema wananchi kuanzisha shughuli za kilimo, ufugaji na makazi ndani ya hifadhi “mkifanya hivi tutaepuka uhitaji wa kuondoa shughuli ambazo zimeshaanzishwa kama vile kuvunja makazi, kufyeka mazao au kukamata mifugo”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii ifanye ufuatiliaji wa malalamiko ya wananchi kuhusu tabia ya baadhi ya wahifadhi kuswaga mifugo na kiingiza hifadhini kwa lengo la kuitafisha na kujipatia fedha. “ Chukueni hatua kali kwa watumishi watakaobainika kufanya vitendo hivyo”

Katika Hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Wananchi wenye malalamiko ya kunyang’anywa mali, mifugo au kujeruhiwa watoe taarifa ya matukio hayo kwa wakati katika vituo vya polisi na Mamlaka za Wilaya ili Serikali iweze kuchukua hatua. “Nitoe rai kwa wananchi wenzangu kuzingatia sheria hususan zinazosimamia masuala ya uhifadhi na kuheshimu mipaka”.

Aidha, Mhe. Kassim Majaliwa amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kutoa elimu kuhusu vigezo vya kulipwa kifuta machozi na kifuta jasho baada ya athari za matukio ya Wanyamapori ili viendane na uhalisia

WAZIRI MKUU, amesema Wahifadhi (CSR) waimarishe mahusiano ya ujirani mwema na kutoa elimu kwa wananchi wanaopakana na hifadhi kuhusu manufaa ya uhifadhi endelevu unaohitajika kushirikisha miongoni mwao na kwa kadiri itakavyofaa wachangie katika shughuli za kijamii na maendeleo ya vijiji jirani ili kufanya ulinzi wa maeneo hayo uwe imara.

Vilevile, Vijiji vinavyokaliwa na watu vilivyopitiwa na Mawaziri Nane (8) havijafutwa kwa kuwekwa kwenye hifadhi na badala yake vimeongezeka na kufikia Vijiji 998.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-04-27 at 14.50.56.mp4
    13.6 MB
  • WhatsApp Image 2023-04-27 at 15.05.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-27 at 15.05.29.jpeg
    209.2 KB · Views: 3
  • FutfqYqX0AA66N-.jpg
    FutfqYqX0AA66N-.jpg
    141.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-04-27 at 15.08.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-27 at 15.08.07.jpeg
    50.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom