Mbunge Kamonga: Maeneo mengine Vijana wanawaza kuandamana, sisi wananchi wa Ludewa wanawaza kuvuna mahindi

Mbunge Kamonga: Maeneo mengine Vijana wanawaza kuandamana, sisi wananchi wa Ludewa wanawaza kuvuna mahindi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga, amesema wakazi wa Ludewa wameendelea kuweka juhudi kwenye kilimo hususani cha mahindi na kuiomba Serikali kuendelea kufikisha fedha kwenye wilaya hiyo ili kuboredha miundombinu ikiwemo ya barabara.

Kamonga ameeleza hayo wakati akizungumza na wakazi wa Ludewa mjini mbele ya Waziri wa wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo.

"Wananchi wa Ludewa mwaka huu wamepata mahindi mengi sana na wenzetu maeneo mengine vijana wanawaza kuandamana sisi watu wanawaza kwenda kuvuna mahindi yao ili solo likija waende kufanya biashara", amesema Kamonga.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Mbunge Kamonga ameiomba serikali kuendelea na ujenzi ikiwemo wa Barabara ya Njombe-Ludewa-Manda ili wakazi wa wilaya hiyo waimarike kiuchumi.


 
Back
Top Bottom