Mbunge Kampala: Dar ni Kiwanda kikubwa sana cha kuzalisha Mashoga, nini kauli ya Serikali?

Mbunge Kampala: Dar ni Kiwanda kikubwa sana cha kuzalisha Mashoga, nini kauli ya Serikali?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria dhidi ya vitendo vyote vinavyokiuka maadili, mila na desturi za Kitanzania, ikiwemo biashara ya ukahaba na makosa mengine yanayohusiana na maadili ya Jamii.


Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Katavi, Thomas Kampala Maganga, Bungeni Jijini Dodoma Juni 15, 2026 aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu Watu wanaojihusisha na ushoga katika Jamii, Katambi amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanyia kazi taarifa zinazotolewa na Wananchi kuhusu vitendo vinavyokiuka Sheria na kuchukua hatua pale ushahidi unapopatikana.

“Tumeendelea kusimamia Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ambayo inaeleza kuhusu makosa ya ujinai yanayovunja maadili ya Kitanzania kwa mujibu wa mila na desturi, katika Sheria hiyo, vifungu vya 139 hadi 147 vinaeleza makosa yanayohusiana na kujamiiana kinyume na utaratibu na katika kipindi chote tumeendelea kuchukua hatua kwa kadri ushahidi unavyopatikana,” amesema Katambi.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha operesheni na uchunguzi wa makosa hayo, huku akitoa onyo kwa Watu wanaoendesha madanguro na biashara ya ukahaba kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Natumia fursa hii kupitia Bunge hili kutoa onyo kwa wale wote wanaoendesha madanguro ni kinyume cha Kifungu cha 147 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu na Kifungu cha 148 kinakataza Mtu kuwa na dangulo, kunufaika au kupata kipato kupitia biashara ya ukahaba”

 
Chanzo cha ushoga ni nin kwan?
Kuuzungumzia ndio chanzo na kujifanya wanataka kuzuia ndio chanzo cha pili ambacho kinaonyesha kwamba wewe pia ni shoga mstaafu yaan umewahi kufirwa, kwa hio ni sawa na unaona moto unawaka wewe unaenda kuzima moto unaacha kwenda kuzima chanzo cha moto hii ndio shida ya kua na viongozi vilaza
 
Huyu naibu waziri mzanzibar anafaidi tu kodi zetu za Tanganyika lakini kodi zao kule zanziba hawataki tuzitumie watanganyika.awamu hii imekuwa ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom