GE2025 Mbunge Kasalali Mageni atangaza kung’atuka na kutoendelea na masuala ya siasa

GE2025 Mbunge Kasalali Mageni atangaza kung’atuka na kutoendelea na masuala ya siasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge wa Jimbo la Sumve mkoani Mwanza, Kasalali Mageni anayemaliza muda wake ametangaza kung’atuka na kutoendelea na masuala ya siasa huku akibanisha kuwa hatagombea tena na ubunge wa jimbo hilo.

Kasalali ametangaza leo Julai 2 mwaka huu na kueleza kuwa kwa sasa anataka kupumzika kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa kile alichodai muda wa miaka mitano imemtosha.

Amesema sababu zilizosababisha kuachana na siasa ni baada ya kutekeleza ahadi alizoahidi mwaka 2020 - 2025 ikiwemo masuala ya afya, elimu, maji, nishati na barabara.

Amesema ni muda wa kumuachia nafasi mtu mwingine kugombea aweze kuendeleza mazuri yaliyofanyika kwa miaka mitano.

Mbunge huyo ameeleza kuwa licha ya serikali kufanya kazi kubwa katika upande wa afya na elimu bado jimbo hilo linakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama pamoja uhitaji wa miundombinu ya barabara za kiwango cha lami.

Screenshot 2025-07-02 231502.png
 
Wasukuma wameanza kujtambua, huyu ama kahitimisha vizuri sana hapo mwisho.
 
Back
Top Bottom