GE2025 Mbunge Katani Ahmed: Tandahimba ya sasa barabara zinafanana na Doha, Qatar

GE2025 Mbunge Katani Ahmed: Tandahimba ya sasa barabara zinafanana na Doha, Qatar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
FB_IMG_1751324187145.jpg
FB_IMG_1749451296938.jpg
Hizi kenge za Ccm zinatuchukulia powa sana.
 

Attachments

  • FB_IMG_1749396463396.jpg
    FB_IMG_1749396463396.jpg
    117.8 KB · Views: 17
Hizo barabara ziko wapi tulinganishe na Doha, bahati nzuri za doha tunazijua
 
Mbunge wa Tandahimba 2015 - 2025, Katani Ahmed Katani amesema maendeleo makubwa ya miundombinu katika jimbo lake yameifanya Tandahimba kufanana na miji ya kimataifa kama Doha, Qatar.

"Leo ukienda Tandahimba kuanzia saa moja jioni, chukua selfie, upige picha kwenye barabara za Doha, Qatar, halafu upite barabara za Tandahimba na uweke kwenye mtandao — huwezi kuona tofauti," alisema Katani.

Ameongeza kuwa Tandahimba mjini sasa ni miongoni mwa miji inayoongoza kwa taa za barabarani mkoani Mtwara. "Usiku ukipita barabarani mji wangu mimi sasa ni katika miji, ukienda mkoa wa Mtwara unaongoza kwa taa za barabarani. Unaokota mpaka sindano, huna sababu ya kutumia baiskeli na kuwasha taa, huna sababu ya kuendesha gari na kuwasha taa. Utawasha taa kwa sababu ni takwa la sheria za barabarani, ikifika saa 12 uwashe taa."

Aiseee uungwana ni vitendo ,nafuta kauli ,nimeona youtube video ya Vloger Chinduli The Navigator akionyesha mji wa tandahimba ,sikutarajia kama papo vile ,ni kweli Jamaa ametijahihi mji umepangika vizuri na kuna Taa za barabarani ,sehemu kubwa city center imepigwa lami.
 
Back
Top Bottom